- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
NA THOMMY KUNDY TUPAMBANE.BLOG
Mechi
baina ya Azam na Yanga kuwania ngao ya jamii kuashilia ufunguzi wa ligi
kuu Tanzania bara,inachezwa septemba 14 mwaka huu. Awali mechi hiyo
ilikuwa ichezwe septemba 13 lakini Shirikisho la soka la Tanzania
TFF,likasogeza mbele mchezo huo kwa sababu mbalimbali.
Mechi
hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka wa hapa
nchini,kutokana na maandalizi ya timu hizo.Timu ya soka ya Yanga
kujiandaa na mechi hiyo pamoja na ligi kuu,waliweka kambi kisiwani
Zanzibar ambako walicheza mechi kadhaa za kujipima ubavu.
Huku timu
ya Azam wakiwa hawana muda mrefu tangu watoke nchini Rwanda ambako
walishiriki kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati
maarufu kama kombe la kagame.Kwenye michuano hiyo timu ya Azam waliishia
kwenye hatua ya robo fainali baada yakutolewa na timu ya El Merreikh ya
Sudani kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Tayari
shirikisho la soka Tanzania TFF, limetangaza viingilio kwenye mechi hiyo
ambavyo ni kuanzia sh 5000 mpaka 30000.Tayari joto la mechi hiyo
limeishaanza huku kukiwa na tambo za hapa na pale kutoka kwa timu zote
mbili.
KILA LA HERI TIMU YA YANGA NA AZAM KUELEKEA MECHI HIYO
No comments:
Post a Comment