Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, September 28, 2014

MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA TAHLISO ULIOFANYIKA CHUONI,RUCO-IRINGA


  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter
RAIS_ff746.jpg
Rais wa TAHLISO akitoa maazimio ya mkutano mkuu uliofanyika kwenye chuo cha 
RUCO(Picha na Thommy kundy)
NaThommy kundy
MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya 
 juu,kupitia Afisa Habari wake tareh 19 agosti 2014,Ni kwamba mpaka kufika 
tarehe 31 julai 2014,jumla ya waombaji 58,037 walikua wameomba wameomba 
mikopo.Bodi ya mikopo walitoa Takwimu kutokana na Bajeti finyu kati ya 
waombaji 58,037 wa mikopo,Bodi itatoa mikopo kwa waombaji 30,000 pekee 
sawa (51%) ,na waombaji 28,037 sawa na 49% hawatapata mikopo,Karibu nusu 
ya waombaji wote watakosa mkopo ingawa watajiunga na Elimu ya juu
MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA TAHLISO
Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kwamba wote walioomba mikopo 
mwaka huu yaani wanafunzi 58,037 wapewe mkopo wote kama tu watakua 
wamedahiliwa na Tume ya vyuo vikuu kuingia Elimu ya juu,Hili ni jambo la 
dharura na tunaitaka serikali kuhakikisha kufanya hivo kwani wote ni watanzania 
wanaostahili mgawanyo sawa wa keki ya Taifa
MATABAKA KATIKA KUTOA MIKOPO
Kumekua na kitu kinachoitwa kozi kipaumbele na zisizo kipaumbele katika 
utoaji wa mikopo,Hili limeleta matabaka miongoni wa wanafunzi wa Elimu ya 
juu ambao wote ni watanzania,Nchi hii bado iko nyuma kiuchumi na kimaendeleo,
Taifa linahitaji wasomi waliofuzu katika kada zao ili kusukuma mbele maendeleo 
ya Taifa,Nchi hii inahitaji wataalamu katika Nyanja zote walimu,wahandisi,
wanasheria na wataalamu katika Nyanja zote na sit u katika Uhandisi na 
Udaktari pekee ingawa tunakiri kada hizi zina upungufu(t.k)
MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA TAHLISO
Mkutano mkuu wa TAHLISO kwa niaba ya wanafunzi wote wa Elimu ya juu 
umezimia kuitaka serikali ihakikishe mikopo inatolewa kwa wanafunzi wote wa 
Elimu ya juu wa Taifa hili bila kujali kozi kipaumbele na zisizokipaumbele.
Mkutano mkuu umezimia hili lianze kutekelezwa mwaka huu wa masomo 
yaani 2014/15,Yaani wanafunzi wote waliokatika Elimu ya juu wapewe 
mikopo,kudahiliwa kuingia Elimua ya juu kiwe ndicho kigezo cha kupata 
mkopo na si vinginevyo.
Mfano tuna wanafunzi........... wa chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Dodoma 
wanaoingia mwaka wa waliomba mikopo mwaka jana na wote hawakupata,
Mkutano mkuu wa TAHLISO umezimia mfano wa wanafunzi hawa wa CBE 
na wote walio katika vyuo mbalimbali wapewe mikopo mwaka huu wa 
masomo 2014/15
MIKOPO KATIKA ELIMU YA KATI
Wanafunzi wanaosoma stashahada(Diploma) katika Taifa hili wote wamekua 
hawapewi mikopo kama ilivyo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu yaani vyuo 
vikuu wanaosoma Shahada.Elimu ya kati ndiyo injini ya maendeleo ya Taifa 
lolote lile kwani katika ngazi hii Elimu ya Ufundi,Elimu ya awali ya udaktari,
uuguzi,ufamasia,ugavi na nyingine hutolewa na wahitimu katika ngazi hii wengi 
huenda kufanya ngazi maeneo ya pembezeno mwa nchi ambayo yamesahaulika na 
yanahitaji msaada mkubwa wa wataalamu,yaani wengi wao huenda kufanya kazi 
vijijini waliko watanzania wengi na ambako hali ya maisha ni duni,kutotoa mikopo 
kwa wanafunzi hawa ni kudidimiza maendeleo ya Taifa
MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU
Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kwamba serikali ihakikishe wanafunzi 
wote katika ngazi hii wanapewa mikopo kama ilivyo kwa wenzao walio katika 
Elimu ya juu wanaosoma shahada katika kada mbalimbali
DHANA YA 100% YA MIKOPO KWA VYUO BINAFSI
Wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu vya Binafsi wamekua wahanga wakubwa 
wa kitu kinacoitwa 100% ya mkopo.Wanafunzi hawa ambao wengi wao ni wale 
wanaosoma kada ya Afya yaani Udaktari,uuguzi,ufamasia na utaalamu wa maabara 
katika vyuo binafsi wamekua wanapewa sehemu ndogo tu ya gharama halisi 
wanazolipa huku wakiitwa wanapewa 100%.Wanafunzi katika vyuo vya KCMC,
Chuo cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki(HKMU),CUHAS-Bugando,St.Francis 
Ifakara,Chuo cha kimataifa cha Tiba na Teknolojia(IMTU) wanalipa ada na 
michango mikubwa sana ambao wanalazimika kuongeza kiwango kikubwa 
kikubwa kama michango binafsi huku ikiwepo dhana ya kwamba wanapewa 100%.
Tunaitaka serikali itoe 100% kwa wanafunzi hawa wa vyuo hivi ili dhana ya 100% 
 itekelezwe,kwani kwa sasa wanapewa kati ya 40% na 60% tu,ya michango yote 
vyuoni,wanalazimika kuongeza zaidi ya Milioni 5 mpaka Milioni 6 kama mchango 
binafsi(self-contribution) kiwango ambacho ni changamoto kubwa kwani wanafunzi 
wamelazimika kuacha masomo kwenda kutafuta fedha,kushindwa kufanya mtihani 
na kushindwa kulipa gharama hizi kubwa.
MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA TAHLISO
Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia,Tunaitaka serikali itoe 100% ya kweli 
kwa wanafunzi kwa vyuo tajwa hapo yaani rejea juu,Kuanzia mwaka huu wa 
masomo hilo litekelezwe mara moja kabala wanafunzi hawarudi vyuoni.
KIWANGO CHA MKOPO
Kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kwa zaidi ya 100% hivyo 
kupelekea wanafunzi Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kuitaka 
serikali kuongeza kiwango cha fedha ya kujikimu kutoka Shs.75,000/-
 kwa siku iliyopo sasa Hadi kiwango cha Shs.15,000/- kwa siku.
CHANGAMOTO YA ADA VYUONI
Kwa kuwa Tume ya vyuo vikuu(TCU) ndiyo imepewa mamlaka kisheria na 
sheria ya vyuo vikuu na.7,2005 kusimamia Elimu ya juu nchini,Na kwa kua 
TCU ilisambaza waraka kwa vyuo vyote tarehe 4 Julai 2014 kuvitaka 
kutopandisha viwango vya Ada,Mapaka pale Mfumo wa upangaji 
Ada wa pamoja(student Unit Cost) utakapoanza kufanya,na kwa waraka ule 
na maelekezo yale yamekiukwa.
Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kuitaka TCU kutoa waraka na 
maelekezo mengine kwa vyuo hivi ambapo nakala zitatolewa pia kwa 
TAHLISO kuvitaka vyuo hivi kufuata maelekezo ya Barua ya tarehe 4 
Julai 2014 kwa vyuo hivi,Barua iliyovitaka visitisha uongezwaji wa ada.
Kwani Mkutani mkuu wa TAHLISO umetoa muongozo kwa wanafunzi 
wote wa Elimu ya juu katika Taifa hili kuhakikisha analipa kiwango cha Ada 
ambacho hakina ongezeko lolote tofauti kwani Hakuna chuo kilichoongeza 
ada na Ongezeko lile likapitishwa(approved) na Kamisheni ya TCU(TCU 
Commission),TAHLISO pamoja na wajumbe wa Mkutanio Mkuu pamoja na 
wanafunzi wa vyuo wahanga St.Francis Ifakara,KCMC,CUHAS-Bugando na 
wanafunzi wote wa Elimu ya juu kuhakikisha hakuna anayelipa ongezeko na 
mwanafunzi yeyote atakayesumbuliwa kwa ajili wanafunzi wa Elimu ya juu 
wote wa Elimu ya juu wataungana kumtetea kwani ni uonevu
MAFUNZO KWA VITENDO
Kumekua na Baadhi ya wanafunzi ambao hawaendi kufanya mafunzo kwa 
vitendo(Fieldwork) mpaka wanahitimu masomo.Mkutano mkuu wa TAHLISO 
 umeazimia Mwanafunzi yeyote wa Elimu ya juu anyetakiwa kwenda Field 
kwa mijibu wa Mtaala na kama Mtaala una makosa urekebishwe ili wanafunzi 
wote wawezwe kwenda Field hatuwezi kua na wasomi na wataalamu ambao 
hawajifunzi kwa vitendo wakiwa vyuoni.
Mfano chuo Kikuu cha Dodoma kitivo cha SOCIAL SCIENCE AND 
HUMANITIES,Tangu mwaka 2011 wanafunzi hawa waliandamana 
kudai kwenda field na hawakusikilizwa na baadhi yao walisimamishwa 
masomo,Mwaka huu fedha ya field ilipelekwa kutoka Bodi ya mikopo 
kwa ajili ya wanafunzi hawa,Lakini baadaya ilirudishwa Bodi ya mikopo 
kwa madai ilipelekwa kawa makosa kwa kua wanafunzi hawa hawendi 
kinyume kabia na mtaala.
Mkutano Mkuu umeazimia wanafunzi wote wanaotakiwa kwenda field 
kwa mujibu wa mitaala na wale amabo mitaala yao ina makosa irekebishwe 
na wote waende field na wapewe fedha ya kujikimu huko kama ulivyo 
utaratibu,Mwaka huu ewa masomo Mkutano mkuu wa TAHLISO 
umeazimia wana funzi wote wa UDOM,College of Humanities and Social 
Science kozi za Project Planning na Law waende field kama ulivyoutaratibu
 na si vinginevyo,TAHLISO haitakubali pamoja na wanafunzi wote wa Elimu 
ya juu kuona kuna wanafunzi wote wakiwemo hawa wa UDOM haweandi 
field,Bali Mkutano mkuu umeazimia kwamba mwanafunzi yeyote wa Elimu 
ya juu aende field kwa matakwa ya mtaala(Carricullum) ya kozi anayosoma
KUHUSU QUALITY ASSURANCE
WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TAHLISO KUKUTANA KWA 
DHARURA NA WAZIRI WA ELIMU
Mkutano Mkuu wa TAHLISO umeazimia mambo mawili makubwa,Moja:FAX 
tayari imetumwa leo asubuhi kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi 
Dr.Shukuru Kawambwa kwa mambo mawili;
(1).Moja,Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia MAAZIMIO haya yafike 
katika ofisi ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu kutekelezwa 
kwa wakati muafaka MAAZIMIO HAYA na tupate majibu yake ndani ya 
masaa ishirini na nne(24).
(2).Pili,Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kwamba katika FAX 
iliyotumwa kwa waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Imeambatana na 
kuomba kukutana(Appointment) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi 
siku ya jumanne,tarehe 30 septemba 2014 pamoja na Wajumbe wa Mkutano 
ili kujadili mambo kadha wa kadha yahusuyo wanafunzi wa Elimu ya juu.
USHAURI WA MKUTANO MKUU WA TAHLISO KWA SERIKALI YA 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mkutano Mkuu wa TAHLISO umeazimia kuishauri serikali iyasimamie 
yafuatayo ili kuboresha mapato ya serikali ambayo yatapelekea Bajeti ya 
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kua ya kutosha na Baadaye kupelekea 
Bodi ya mikopo kupata kiasi cha kutosha ili waombaji wote wa 
mikopo waweze kupata;
(1).Ukwepaji Kodi
(2).Misamaha ya kodi
(3)Mishahara hewa
(4)Ukusanyaji mzuri wa kodi
(5).Mkakati wa kufufua viwanda vilivyokuwapo tangu uhuru zaidi ya 400
(6).Fedha zinazokopwa na serikali zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo 
ili kuinnua uchumi wa Taifa

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG