Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, September 9, 2014

majeshi yatuhumiwa kubaka somalia

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 


Shirika la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch, limetuhumu majeshi ya Umoja wa Afrika yaliyopo Somalia kwa kubaka wanawake na wasichana, na pia kudai ngono ili kuwapa chakua cha misaada.(MC)
Taarifa iliyoandikwa kutokana na ushuhuda uliotolewa na wanawake na wasichana ishirini na mmoja, imesema baadhi ya wanajeshi kutoka Burundi na Uganda walitumia ahadi ya kuwapa misaada ya kibinaadam ili kuwashawishi wanawake na wasichana kufanya nao tendo la ndoa.
Human Rights Watch imesema wanawake walinyanyaswa kijinsia wakati wakitafuta huduma za afya au maji katika kambi za Umoja wa Afrika. AU imesema itachunguza tuhuma hizo. Wanajeshi wapatao elfu ishirini na mbili kutoka mataifa kadhaa yamekuwa yakipambana na al-Shabaab nchini Somalia kwa miaka saba iliyopita.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG