Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, September 12, 2014

mapigano



Watu 19 wauawa
kwenye mapigano
makali yaliyojiri nchini
Somalia
Kwa akali raia 19 wameuawa na wengine
wasiopungua 33 kujeruhiwa, baada ya kutokea
mapigano makali kati ya vikosi vya serikali ya
Somalia na wanamgambo wa kundi la al
Shabaab katika eneo la kaskazini mwa mji mkuu
wa nchi hiyo, Mogadishu. Taarifa zinasema
kuwa, wanamgambo 34 wa kundi la al Shabaab
pia wameuawa kwenye mapigano hayo. Kundi la
al Shabaab linaendelea kudai kwamba
litaendeleza mapambano yake dhidi ya majeshi
ya serikali ya mpito ya Somalia, hadi pale vikosi
vyote vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika
vitakapoondoka nchini humo. Wakati huohuo,
taasisi moja ya kutoa misaada ya kibinadamu
yenye makao yake Geneva imeeleza kuwa, watu
wasiopungua elfu tano wamejeruhiwa na kulazwa
katika hospitali za Mogadishu, wakiwemo
wanawake na watoto 1,900 katika kipindi cha
Januari hadi Septemba mwaka huu. Nchi za
Uganda na Burundi ndizo pekee hadi sasa
zimeshaitikia wito wa Umoja wa Afrika wa
kutuma wanajeshi wake wa kulinda amani nchini
Somalia.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG