Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, September 26, 2014

Mchinjaji wa IS atambuliwa


Mkurugenzi wa FBI James Comey
Mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye 
 huficha sura yake ambaye ni muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati akiwachinja mateka 
watatu kwenye video inayo nadi wanamgambo wa dola ya kiislam IS.
Pamoja na hayo Bwana Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja 
jina lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya mji wa 
London, na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo umefanikishwa kwa msaada
 mkubwa wa marafiki wa kimataifa.
Muuaji huyo wa waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa 
kujitolea David Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye mitandao na wanamgambo
 hao wa dola ya kiislam na kusaidia kufanya maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa jihad

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG