Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, September 26, 2014

CHADEMA, POLISI BUSARA ITUMIKE




Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' na 
Kiongozi wa 
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,  Freeman Mbowe,
Na Ojuku Ibrahim
MAAZIMIO ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) 
ya kuitisha maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima kupinga kuendelea kwa 
vikao vya Bunge Maalum 
la Katiba (BMK) na baadaye kauli kali ya Jeshi la Polisi ya kukataza kitendo hicho na 
kutishia kutumia 
nguvu kuyazima, yanaweza kusababisha maafa kama busara hazitatumika kwa pande 
zote mbili.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kada na vyama mbalimbali waliohojiwa 
 kufuatia kuitwa polisi na kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe 
aliyetoa kauli hiyo wakati wa 
mkutano wa chama hicho hivi karibuni.(T.K)
Chacha Maiya, aliyejitambulisha kama mwanafunzi wa sheria kutoka Chuo 
Kikuu Huria, 
alisema ingawa ni haki ya msingi kwa wananchi kuandamana, lakini tafsiri 
inayotokana na 
maneno ya 
Mbowe ni kama inayoashiria vurugu kutoka kwa wafuasi wake, jambo ambalo 

halikubaliki.
“Ni kama vile Mwenyekiti Mbowe anawahamasisha wafuasi wake kufanya vurugu. 
Nadhani kulikuwa na haja ya kuwa makini katika kutoa matamshi hasa unapotaka 
kuhamasisha
 umma, sasa suala 
la msingi ni kwa wao kusitisha maandamano yao na kufikiria njia nyingine ya
 kuwasilisha 
ujumbe wao kwa Rais 
au Bunge,” alisema.
Akizungumzia sakata hilo, kiongozi mmoja wa Chadema aliyeomba hifadhi ya jina lake, 

 alisema kitendo cha polisi kuzuia maandamano yao hakiwezi kulipa uhalali Bunge 
Maalum kuendelea, isipokuwa 
wanazidi kuchochea ari ya wananchi katika kutafuta haki yao.
“Ipo siku watu watasema basi, imetosha, hivi vitisho vina mwisho wake, 
polisi wanataka
 kuingilia siasa kwa kuilinda CCM, lakini watambue kuwa hakuna sheria 
inayowapa mamlaka
 ya kuzuia
 maandamano ya kisiasa, walichopaswa kufanya, ni kutoa maelekezo ya 
namna ya kufanikisha 
maandamano hayo
 ili yatawaliwe na amani, siyo kupiga watu mabomu,” alisema.
Tokea kutolewa kwa maazimio hayo ya Chadema, wafuasi kadhaa wa chama 
hicho 
wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini na wengine kufikishwa 
mahakamani,
 baada ya kujaribu kuandamana na 
polisi kutumia nguvu kuwazuia.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG