Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, September 1, 2014

Mmasai Ole Sosopi, ajitosa kugombea M/Mwenyekiti BAVICHA Taifa

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 
Ole Sosopi katika moja yab mikutano yake
Mjasili haachi asiliye Ole Sosopi akipandisha mori kijijini kwao

Na Mathias Canal, Kwanza jamii-Iringa
Anaitwa Patrick Ole Sosopi, Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani.
Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). Kwa sasa kazi zake ni kufuga ng'ombe. Ni Baba wa mke mmoja na mtoto mmoja.
Ni mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA Bara- Taifa.Historia yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna shaka katika vipindi mbalimbali vya maisha yake.
Historia yake ya uongozi ilianzia akiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu cha RUCO ambapo alikuwa waziri wa Fedha kwenye serikali ya wanafunzi 2011/2012.
Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.
Ole Sosopi ni mojawapo wa waanzilishi wa CHASO mkoani Iringa, harakati zake katika jimbo la Ismani na mkoa wa Iringa kwa ujumla kila mtu anazijua. Ameshiriki katika mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa wa Iringa pamoja na Mbeya.
Wakati Daudi Mwangosi akiuliwa kikatili na jeshi la Polisi alikuwa umbali tu wa mita kumi akishuhudia.
Aliaminiwa na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na kushauriana na familia yake na vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ameona agombee nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara.
Ingawa ni mojawapo wa wasomi wachache kwenye jamii ya yao, ni mtu ambaye usomi wake haujamfanya asahau mila na tamaduni za nkimasai. Chakula chake, mavazi yake, desturi yake ya maisha ya kila siku ni desturi za kwao na zenye kuhuwisha Utanzania.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG