Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, September 2, 2014

Q - CHILA AFUNGUKA UJIO WAKE MPYA

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 

Nguli wa Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ akifunguka ndani ya studio za Global TV Online.
TUNAENDELEA na simulizi ya staa wa Bongo Fleva, Aboubakar Shaaban Katwila ‘Q- Chillah’, wiki iliyopita iliishia pale alipoelezea juu ya kilichomtokea katika msiba wa msanii wa filamu, Adam Kuambiana, alisema marehemu ndiye aliyegundua kipaji chake cha kuigiza, songa nayo sasa… 
(Anainamisha kichwa chini na kuinua huku machozi yakimlengalenga)
...niliogopa sana lakini niliona sanaa ni sanaa, nilikwenda kumuona na akanijenga kisanii. Alinipa nicheze movie ya JB inaitwa Hukumu ya Ndoa Yangu ambayo yeye (Kuambiana) alikuwa muongozaji (Dairekta), alinipatia vipande vinne, nikavicheza vizuri.GPL (P.T)
Kipindi ambacho nilikuwa naye kambini naweza kusema nilikuwa mtu pekee aliyekuwa akiniambia matatizo yake kwa pale kambini, siku ya mwisho wa uhai wake nilitoka katika chumba chake na kumuacha vizuri tu na kuhamia chumba kingine, baada ya muda wenzangu walinifuata na kuniambia kuwa Kuambiana amezidiwa, nilijua ni utani kwani nilizoea matani naye sana…
(Anakatisha maongezi, kimya cha ghafla kinatawala huku akitafakari kitu, machozi yanaanza kumtoka, macho yanabadilika na kuwa mekundu, kisha anaendelea)
…hadi tunampeleka hospitali bado nilikuwa nikishangaa na kuona imekuwaje ghafla vile, lakini kufika tu nje ya hospitali akaaga dunia. Niseme namshukuru tu kwa mchango wake mkubwa aliouonyesha kwangu.

Q-Chillah akifikiria jambo wakati akihojiwa na Global TV Online.
Nani anakusimamia kwa sasa?
Kampuni ya QS Muhonda ndiyo nimesaini nao mkataba, wanashughulika na mambo yote ya kuniandalia shoo. Nimekaa na wadau chini na kampuni hii na kuelewana kwanza kutafuta amani. Kwa sababu siwezi kuanza kufanya biashara bila kuwa na amani, nataka niwaambie kwanza watu nataka kuwa na amani kwanza ndipo niwaeleze matatizo yangu wajue wapi nimekosea.
(Anajiweka vizuri na kushika vidole vya mikono)
…jana nimeposti habari ya kurudi kwangu Bongo5 lakini huwezi amini nimepata shoo mbili mwezi Desemba kutoka Nairobi zikitaka kufanya kazi na mimi huku nyingine zikiulizia kama nimekufa kwani walikuwa wakisikia vitu vingi vibaya kuhusu mimi…
(kimya kinatawala, anaonekana kama kutafakari kitu kisha anaendelea kuzungumza)
…Nipo hai sijafa, nilikuwa mbali na vyombo vya habari na huo nakiri ni ujinga ambao nilikuwa nikiufanya. Mkiwa kama kaka zangu, dada zangu na waandishi ambao mnanielewa vizuri, mnatakiwa mnisamehe kama walivyo binadamu wengine, najua nimekosa.
(Anatikisa kichwa kwa masikitiko huku mikono akiitumia kufuta paji lake la uso)

Q-Chillah akipozi na Wahariri wa Magazeti ya Global Publishers, Erick Evarist (kulia) na Siafel Paul (kushoto) baada ya mahojiano.
Atomic Band iliishia wapi?
Wakati namiliki Bendi ya Atomic nilikuwa na miaka 17 au 18. Kwa mtu ambaye hana elimu ya kutosha hawezi kusimamia pale nilipokuwa nimesimama. Sikuweza kujua naiendeshaje kiushindani kutokana na kuwepo kwa bendi kubwa kama Msondo, Twanga Pepeta na kadhalika. 
Nilikuja kuhamia Kenya, vyombo nilivigawa kwa kanisa kwa kuona naenda kuanza maisha mapya mengine hivyo kugawa vyombo ni kama kupata baraka za Mungu na ndiyo maana leo hii nipo hapa...
(Ananyamaza tena kisha baada ya muda anaendelea)
..Nilirudi nakuja kukaa na TID (Khalid Mohamed) na kuweka fungu na kumwambia aende Dubai kutafuta vyombo na akavileta, lakini kama binadamu ana tofauti zake kama vile itikadi na malezi na kadhalika. Nilipokuwa na TID nilikuwa sijui kama anatumia unga. Nilijikuta naanza kutumia unga baada ya kuwa na maisha magumu, siyo kwamba nilidhamiria…
(kimya kinatawala)
… yote yamepita na sasa naendelea na maisha mapya baada ya kuachana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka miwili.
Ruge na Ridhiwani walinipigania na kunifanya niache madawa ya kulevya, waliniambia watanipa nafasi nyingine ya kufanya muziki.

Q-Chillah akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally.
Kuna tetesi kuwa ulitaka kujiua kwa sumu, ni kweli?
(anaonekana kushtuka, anavuta pumzi kisha anajibu)
Haya huwa yanatokea kutokana na maisha magumu. Namshukuru Mungu, Albert Mangwea, Chuji na Niyonzima walinisaidia sana, nilitaka kujinyonga kwa sababu nilikuwa sina ninachoogopa, nawashukuru sana hawa watu niliowataja. 

Ngoma gani ambayo unaipenda sana?
(Swali linaonekana kumuingia, anakuna kichwa sambamba na kukohoa kisha anajibu)
Ngoma ninayoipenda ni  Dreamer,  niliiandika nikiwa na kibatari usiku sana.
Q-Chillah akiwa nje ya ofisi za Global Publishers.

Ilikuwaje ukakosana na baba yako, unafafanuaje hilo?
(Kimya kinatawala kwa muda, anainama chini kisha anawaangalia waandishi na baada ya hapo anaanza kujibu)
Ni mambo ya maisha, lakini mzazi ni mzazi na tulisuluhishwa na wazee wa msikiti na wa kanisa. Kwa mara ya kwanza baba yangu alikuja kuniona na kulala kifuani kwangu kwa sababu nililelewa na mama ambaye siyo mzazi wa kunizaa. Baba aliambiwa, alipigiwa simu na viongozi baada ya kuniona nipo hovyo na leo huwezi kuniita kwenye shoo bila kuongea na baba. Namshukuru Mungu hadi sasa, nina watoto watatu na kila mmoja ana mama yake.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG