Ndugu zangu,
Ni
Ipelanya Kulwa, wa kwanza kushoto kwenye picha ya pili. Pichani ni
Harare, Zimbabwe, Desemba, 1989. Ipelanya alikuwa mdogo sana wakati huo,
labda miaka 9 au 10. Mapema mwaka huu niliiweka picha hii kwenye fb,
naye akajitambua. Akanipigia simu. Alishangaa sana kuiona picha yake.
Hakuwa hata na kumbukumbu kuwa nilipata kutembea nae mitaa ya Harare
akiwa na mtoto mwenzake.
Na mimi
niliiweka picha hiyo bila kuwa na kumbukumbu ya majina ya watoto hao. Na
bado ningependa kujua huyomtoto wa pili ni nani. Ipelanya ametaka kujua
zaidi ya wakati huo. Nakumbuka Baba yake alikuwa Mtaalamu wa mawasilino
ya simu. Wakati huo, Zimbabwe iliomba wataalamu wa maeneo mbali mbali
kutoka Tanzania.
Na
hakika, Zimbabwe ilikuwa nchi changa sana.Ilikuwa na miaka 6 tu ya
Uhuru. Na mimi nilikuwa ndio kwanza nimemaliza Form Four pale Tambaza
Sekondari. Tangu enzi nikiwa shuleni , nilipenda sana kufuatilia masuala
ya harakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika. Nilifika Lusaka pia, Zambia.
Nikiwa Zimbabwe sikuishia Harare tu, nilifika maeneo ya vijijini pia.
Nilifika Nyanga, Mberengwa, jirani na mpaka wa Msumbiji, na hata
Bulawayo.
Nikiwa
Nyanga niliona nini maana ya jamii zilizokuwa zikiishi katika mifumo ya
kibaguzi. Mji unakuwa na sehemu mbili; ya Wazungu na Weupe. Kwenye
Township ndiko walikoishi Makabwela.
Kwenye
Maktaba yangu bado nina picha kadhaa za wakati huo. Moja nimepiga nje ya
nyumba ya Ipelanya Harare, nikiwa na dada yake Ipelanya. Ipelanya
ameniambia dada yao amebaki Zimbabwe na ameolewa huko, miaka yenda mbio
kweli!
Hongera Ipelanya kwa kufunga ndoa! Na kule Zimbabwe wanasema Makorokoto!
Maggid
No comments:
Post a Comment