NaThommy kundy- MAELEZO
Mfuko wa
Pensheni (PSPF) umedhamini siku ya Msanii Tanazania itayoadhimishwa
Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City kwa dhumuni la kuwapa
mafunzo wasanii ili waweze kujikwamua kiuchumi.(Victor Simon)
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi amesema kuwa kauli mbiu ya
maadhimisho hayo ni "Sanaa ni kazi" ambayo itajumisha fani mbalimbali
kama vile Taarabu, Muziki wa dansi, ngoma za asili na muziki wa msanii
kutoka nje ya nchi.
Njaidi
ameongeza kuwa fani nyingine ni uchezaji shoo, dansi za mitaani, Bongo
fleva, maonesho ya mitindo ya mavazi, sanaa kwa watoto na maonesho ya
sanaa ya ufundi.
"Tumeona
umuhimu wa kuwepo kwa maadhimisho haya kama vile Mei Mosi, siku ya
UKIMWI Duniani, Siku ya Wanawake Duniani ikiwa ni chachu ya kuhamasisha
wasanii na wadau wake kuthamini sanaa nchini" alisema Njaidi.
Siku ya
Msanii ni mradi uliobuniwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa
kushirikiana na kampuni ya Haak Neel Production ili kuungana na wa sanii
dunia ni kote kuadhimisha siku ya kimataifa ya Msanii inayofanyika kila
mwaka kwa lengo la kumtambua msanii, kazi zake na mchango wake katika
jamii.
Aidha,Njaidi
alisema kuwa PSPF imekuwa mstari wa mbele kutoa fursa kwa watu wote
kujiunga na mfuko kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni.
Zaidi ya
hayo Njaidi amesema kuwa wasanii wamejiajiri na hawana mpango mzuri wa
kuweka akiba ya uzeeni, huvyo PSPF imeamua kushirikiana na BASATA katika
kuandaa Siku ya Msanii kwa kuwapa elimu wasanii wote ili waweze
kujiandaa kwa maisha ya badae.
Mbali na
hayo PSPF inatoa fursa kwa watu wote kujiunga na mfuko kwa ajili ya
kujiwekea akiba ya uzeeni, hivyo kushirikiana na wasanii katika kuwapa
elimu na waweze kujiandaa kwa maisha ya badae
No comments:
Post a Comment