Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, September 27, 2014

Wajumbe wa Bunge watishiwa maisha


Ukumbi-wa-Bunge-la-Katiba_73be3.jpg
Siku tatu kabla ya Bunge la Katiba kuanza kupigia kura Rasimu ya Katiba 
 inayopendekezwa,
 watu wasiojulikana wameanza kusambaza vitisho vya kuwatia hofu wajumbe 
wa Bunge hilo.
Watu hao wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbalimbali ya mji wa 
Dodoma 
usiku wa kuamkia jana, wakiwataka wajumbe kutoingia bungeni vinginevyo 
yatakayowapata watajuta, huku wajumbe kutoka Zanzibar wakitishiwa kwa
 ujumbe 
wa simu kupitia mtandao wa WhatsApp.
Tayari, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd ametoa kauli 
 kuhusu vitisho hivyo akisema Serikali itachukua kila hatua kuhakikisha wajumbe 
kutoka visiwani humo ambao wamekuwa wakipokea vitisho wanakuwa salama.
Mbali na kusambazwa kwa karatasi hizo, maandishi mekundu yamechorwa katika
 kuta za jengo la Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma yakisomeka, "No Katiba. 
No ufisadi."(T.K)
Vikaratasi vilivyosambazwa vinasomeka: "Onyo. Dodoma si mahali pa 
kufuga wezi wa fedha za umma. Utakayeingia bungeni kuanzia kesho (leo),
 yatakayokupata utajuta."
Mkazi wa Dodoma, Sospeter Samwel alimwambia mwandishi wetu jana 
kuwa aliokota baadhi ya vipeperushi hivyo jana saa moja asubuhi katika 
eneo maarufu la kuuzia magazeti linalotazamana na Jengo la CCM.
"Tulikuta hayo makaratasi yametupwa tu ovyoovyo ila baadaye nikasikia 
maeneo mbalimbali mengine nayo yameonekana yametupwa. Sijui nani 
hasa watakuwa wameyasambaza," alisema.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa jana kuhusu 
na maandishi hayo alijibu kwa kifupi "No comment" (sina cha kusema).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime jana alitoa taarifa ya
 maandishi kwa wanahabari akisema jeshi hilo linawasaka watu waliosambaza 
vipeperushi hivyo.
"Wananchi na wageni wapenda amani waendelee na shughuli zao 
kama kawaida kwani polisi tumejiimarisha ipasavyo kukabiliana na 
yeyote atakayekiuka sheria na maelekezo yaliyotolewa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi alitoa onyo kwa 
watu aliodai wanafanya mzaha akisema vyombo vya usalama viko 
macho saa 24. Aliwataka wajumbe kutoa taarifa kwa vyombo vya 
dola wanapoona viashiria vya kutokuwa na usalama.
"Kama ng'ombe mzima tumeshakula tumebakiza mkia tu, niwahakikishie 
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, usalama umekuwapo na 
utaendelea kuwapo.
Wazanzibari kulindwa
Akizungumzia vitisho hivyo hasa kwa wajumbe kutoka Zanzibar, Balozi Idd 
alisema Serikali itachukua kila hatua kuhakikisha wanakuwa salama.
Alisema kuna ujumbe unazunguka katika mitandao ya jamii ukitoa vitisho
 kwa wajumbe wa Bunge hilo na watumishi wa sekretarieti ya Bunge hilo.
"Vyombo vya dola vipo na vitafanya kazi yake. Vinajua vitisho vyote. 
Niwahakikishie wajumbe mtakuwa salama na Serikali itachukua kila hatua 
 kuhakikisha hakuna kitakachotokea.
Hoja 17 za Zanzibar
Akizungumzia kuhusiana hoja 17 ambazo ziliwasilishwa na Mwanasheria 
Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman zenye masilahi ya visiwa 
hivyo, Balozi Idd alisema kati yake 13 zilikubalika na kubakia nne.
Hata hivyo, alisema baada ya kuangalia zaidi Rasimu ya Katiba
 inayopendekezwa 
waligundua kuwa zilibakia hoja tatu tu.
Alizitaja hoja hizo kuwa ni ibara 86 ambayo inasema Rais wa Jamhuri ya
 Muungano atashinda kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50.
Hata hivyo, alisema waliona kwenye Katiba ya sasa jambo hilo liko 
kimya kidogo endapo itatokea mgombea hakupata kura upande wa Zanzibar.
"Tukaona kuwa huyu ni Rais wa Muungano, hivi asilimia 50 yote apate 
Bara legitimacy (uhalali)
 yake kama rais wa Muungano iko wapi?" alisema na kuongeza kuwa vyema 
katika Rasimu ikaingizwa
 kuwa mgombea huyo pamoja na kwamba anatakiwa ashinde kwa zaidi ya 
asilimia 50, basi angalau 
katiba iweke 
kiwango fulani cha kupata upande wa Zanzibar.
Alisema baada ya kutafakari ikakubaliwa Zanzibar angalau mgombea 
huyo apate asilimia 10 au 15. 
Hata hivyo, alisema majadiliano kuhusu suala hilo bado yanaendelea

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG