- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Kauli
hiyo ameitoa leo wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge
hilo huku akisisitiza kuwa huo ni upotoshwaji mkubwa na watu hao
wanapaswa kuangaliwa kuhusu uzalendo wao.(Thommy kundy)
Mhe.
Chawene ameeleza kuwa inasikitisha zaidi hasa pale shutuma
zinapoelekezwa kwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta, kuwa
bunge hilo sasa linaonekana ni mali ya Mwenyekiti wa bunge hilo wakati
si kweli.
"Gazeti
linachukua kurasa tatu hadi nne kuzungumzia habari Sitta king'ang'anizi,
hivi hili bunge lipo kama liliitishwa na Sitta ama na Rais wa nchi?,
hili bunge liko kisheria", alisema Mhe. Chawene.
Aliongeza
kuwa kwa niaba ya Watanzania wanafanya kazi ya bunge hilo kwa mujibu wa
sheria huku akisisitiza kuwa wajumbe waliotoka nje ya bunge hilo
wamevunja sheria na kwamba hawawezi kutafuta uhalali nje ya sheria.
"Wanamlazimisha
Rais avunje bunge hili, Rais wa kufuata utawala bora anavunja kwa
mamlaka yapi? Mamlaka ya Rais yako kwa mujibu wa sheria", alisema Mhe.
Chawene.
Aidha,
ameeleza kuwa Sheria inayoendesha mchakato wa Katiba ni Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ambayo imetungwa kutoka katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yenye hatua tatu zikiwemo hatua ya kukusanya maoni
ambayo Tume ya Warioba ilifanya kazi hiyo na kumaliza, hatua ya Pili ni
bunge hilo kujadili kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwa uwakilishi
uliopo ndani ya bunge hilo na hatua ya tatu ni wananchi kwenda kutunga
Katiba.
"Sisi
hapa tunatoa Katiba inayopendekezwa, inayofuata ni Watanzania kwenda
kutunga Katiba kwa kutunga kwa kupiga kura ya kusema ndiyo au hapana
yale tuliyoyajadili na kuletwa na Tume", alisisitiza Mhe. Chawene.
Aidha,
amewataka watanzania kuwaona watu hao kuwa ni watu wabaya na wasio na
nia nzuri na nchi na kuepuka kuingia barabarani kufanya maandamano ya
kuipinga Katiba hiyo
No comments:
Post a Comment