- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Basi la
Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa
likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana
baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA
COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini
Musoma mchana huu.Watu 25 wamepoteza maisha papo hapo na wengika
kujeruhiwa vibaya sana.
Inaelezwa
kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu
kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332
AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari
moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo
kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza
kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia
mtoni.
Hali
iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo
bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo
kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari
hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja
amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
Basi
la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4
EXPRESS.(P.T)
Umati wa
Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na
kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio hilo
la ajali.
Guldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia
mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na
mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.
Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.
No comments:
Post a Comment