Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, September 23, 2014

ZAIDI ya walinzi 60 wa Kampuni ya KSG kanda ya Iringa wamegoma

YAO_78820.jpg
walinzi walio goma
Baadhi ya walinzi wa kampuni ya kiwango security guards Ltd wakiwa katika ofisi za TUPSE kannda ya nyanda za juu kusini leo kudai mishahara ya miezi miwili. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA

Na Friday Simbaya, Iringa
ZAIDI ya walinzi 60 wa Kampuni ya Kiwango Security Guards Ltd kanda ya Iringa wamegoma kuendelea na kazi ya kulinda minara ya Vodacom wakidai mishahara ya miezi miwili kutoka kwa mwajiri.
Walinzi hao kutoka sehemu mbalimbali ya mkoa wa iringa wakiongea na MJENGWABLOG leo kwa machungu katika ofisi za Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE) Kanda Nyanda za juu Kusini zilizopo mjini Iringa, walisema kuwa wana muomba Rais Jakaya Kikwete awasaidie kutatua tatizo la mwajiri wao ili awalipe mishahara yao ya miezi miwili wanayomdai.
"Mwajiri huyo ni wa kampuni ya ulinzi ya kiwango kutoka jijini Dar es salaam hajatulipa mishahara yetu,kwa kweli hali ni nguu kweli sasa sisi tunafanya kazi kama nyuki tunatumikishwa na hadi sasa tuna miezi miwili hatujalipwa na tunafamilia hatujui familia zetu zitaishi hivyo tunamuomba rais aingilie kati ili tuweze kulipwa mishahara yetu.'walisema
Mzee Ismaili Mpenge (68) ambaye analinda mnara wa Vodacom kadeti uliopo kijiji cha Nyang'oro katika jimbo la isimani iringa alisema kampuni hiyo haijamlipa mishahara ya miezi miwili tangu aanze kazi Julai nne mwaka huu.
Alisema kuwa tangu jana afike mjini iringa kutoka kijijini kwake hajala na nauli yakufika mjini amekopa na kuongeza kuwa hapa mjini hana ndugu na kuomba wasamaria wema wamsaidie sehemu ya kulala anaposubiria malipo.
"Nimetoka katika kijiji cha Nyang'oro tangu jana na sijui hatma na isitoshe tuna watoto wanasoma na mpaka sasa hatujui familia zetu zinakula nini mpaka sasa ... kwa kweli maisha yetu walinzi ni magumu," alisema.
Naye Isaya Mdabagi mlinzi wa mnara wa migori alisema kuwa kwa miezi miwili hatujalipwa mishahara ukizingatia tuna familia tulizoziacha huku nyumbani bila chochote.
Mwajiri aliahidi kulipa mshahara wa mwezi moja na sio mshahara wote kama makubaliano yetu ya kulipwa laki na ishirini lakini amesema kuwa watalipwa shilingi elfu themanini .
Naye Meneja wa Kanda ya Iringa/Mbeya Jacob Omollo alikiri kuwepo kwa madai hayo ya walinzi ya kutolipwa mishahara na kusema kuwa amewasiliana na uongozi kutoka Dar es salaam ambapo alisema wamemtuma mtu kuja kuwalipa.
Alisema kuwa kampuni imeshaanza kulipa mshahara wa mwezi saba na jumatatu watamalizia kulipa mwezi wa nane ambapo walinzi hao walilipwa shilingi 80,000/- badala shilingi laki moja na ishirini (120,000/-).
Kuhusu mkataba, meneja huyo alisema kuwa hajaingia mikataba yoyote na walinzi hao isipokuwa kwa makubaliano fulani ambayo sio kwa maandishi.
Alisema kuwa walinzi hawajalipwa mishahara ya miezi miwili tangu tarehe 04.07.2014.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa TUPSE, Edison Kivelege aliongeza kuwa Iringa ina jumla ya makampuni ya ulinzi binafsi 36 nyingi zikitoka nje ya mkoa, lakini pamoja na hayo kampuni zenye ofisi azizidi kumi (10) na kusababisha kukosa mawasiliano.
Alisema kuwa chama kinapotaka kuwasiliana na wanachama wake kinapata shida ya kuonana na viongozi kwa ajili yakutatua kero za wanachama kwa sababu ofisi nyingi za waajiri zipo Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.
Alisema kuwa kampuni nyingi hapa Iringa zinafanyakazi za udalali kwa sababu hiyo kampuni hizo zinakuwa zinawaajiri walinzi wasiokidhi vigezo ambao wanakuwa na uweledi mdogo kuhusiana na masuala ya ulinzi.
Katibu Mkuu wa TUPSE huyo aliwaasa walinzi kuacha tabia ya kuhamahama makampuni kwa sababu wanaji sababishia kupoteza mafao na uaminifu na kuwahimiza wajisajili na chama hicho ili washiriki katika mabaraza ya majadiliano na waajiri.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG