- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
Na Thommy kundy-MAELEZO
Serikali
wilayani Hai imewaasa wananchi kuachana na tabia ya unywaji wa pombe
uliokithiri ambao unaathiri nguvu kazi pamoja na maendeleo ya jamii na
taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Hai Novatus Makunga
kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Habari Leo toleo Na. 02830
la Ijumaa Septemba mwaka huu yenye kichwa cha habari "Ulevi kwa
wanafunzi wa Hai wamtisha DC".(Victor Simon)
"Si
kweli, hakuna kitu kama hicho wala hakuna taarifa za wanafunzi kunywa
pombe hizo hali inayopelekea kuwa tishio katika wilaya yetu" alisema
Makunga.
Akiongea
kwa njia ya simu kutoka wilayani Hai Makunga alisema kuwa alichosema
wakati wa mazishi ya aliyewahi kuwa Shehe wa mkoa wa Kilimanjaro Ally
Lema alisema wazazi ndio wanaokunywa pombe aina ya gongo na viroba na
sio wanafunzi wa shule za msingi wala sekondari.
Akifafanua
juu ya suala hilo, Makunga alisema kuwa wazazi pamoja na vijana wengi
wanaokaa vijiweni wakiowemo madereva wa "bodaboda" ndio kundi
linalosadikiwa kukithiri katika unywaji wa pombe aina ya gongo na viroba
ambavyo vinatishia kuathiri mfumo wa uzazi.
DC
Makunga aliongeza kuwa pombe hizo ni kali, sio salama na hazina kiwango
ndio maana zinapelekea kupunguza nguvu za uzazi ambapo hata Wachungaji
wa dini mbalimbali wamesema idadi ya watoto wa ubarikio katika makanisa
yao pia imepungua.
Vilevile
wilaya ya nchi nzima inaweza kukosa nguvu kazi kutokana na vijana ambao
ndio nguvu kazi ya taifa kupungua au waliopo kutokuwa na nguvu ya
kufanya kazi inavyopaswa kutokana na hali yao ya unywaji wa pombe hizo
zisizo salama.
Katika
kukabiliana na hali hiyo, Makunga alisema kuwa tayari wilaya yake ipo
katika hatua za mwisho kukamilisha sheria sheria ndogo ndogo inayopiga
marufuku unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi wilayani humo.
Makunga
alisema kuwa kwa sasa Sheria kuu ya Serikali kuhusu unywaji pombe ndiyo
inayotumika ambapo inabainisha kuwa muda wa kunywa pombe siku za kazi
yaani Jumatatu hadi Ijumaa ni kuanzia saa 9: 00 mchana hadi saa 4:00
usiku na siku za Jumamosi, Jumapili na siku za siku kuu ni kuanzia saa
6:00 mchana hadi saa 5:00 usiku ambapo atakayebainika kukiuka utaratibu
huo atachukuliwa hatua za kisheria.
Sheria
hiyo inataja kuwa anayekunywa pombe saa za kazi atapelekwa mahakamani na
kupigwa faini au kifungo cha miezi sita jela au adhabu zote kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment