Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, October 19, 2014

RAIS KIKWETE NA RAIS KABILA WAONGOZA SHEREHE ZA KUHITIMU MAAFISA WAPYA WA JESHI

 Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana Jumamosi Oktoba 18, 2014 
 Maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha 
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi ofisa kadeti Yusup kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko Monduli jana.
 Rais Joseph Kabila wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Mwamtemi baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika mafunzo ya porini wakati wa hafla ya kutunuku kmaisheni baada kumaliza mafunzo ya kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika Chuo cha kijeshi monduli leo.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakisimama kikakamavu wakati nyimbo za taifa za nchi hizo zikipigwa  wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha. Picha na Fred Maro

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG