- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Wachezaji wa Simba wakijadiliana jambo uwanjani
KIKOSI
cha Simba kina silaha moja hatari ambayo kama Yanga watashindwa
kugundua, wataumia ndani ya dakika 35 za mwanzo, lakini dakika za mwisho
za kipindi cha pili Simba huchoka.
Katika
mechi tatu za Ligi Kuu Bara ambazo Simba imecheza chini ya Kocha,
Mzambia Patrick Phiri wamefanikiwa kupata mabao ya mapema kati ya dakika
ya kwanza mpaka 35 za mchezo.
Lakini
pamoja na ubora wao huo dakika za mwanzoni, imekuwa na tatizo la
kuzidiwa na timu pinzani katika dakika za mwishoni ambazo ndiyo
ziliwalazimisha wakatoa sare katika mechi zao tatu za ligi.
Katika
mechi hizo, walipofungua ligi dhidi ya Coastal wakatoa sare ya 2-2,
Simba ndiyo ilianza kufunga mabao yote mawili ambayo yalifungwa na
Shaaban Kisiga dakika ya saba na Mrundi Amissi Tambwe aliyefunga la pili
dakika ya 32.
Lakini
kipindi cha pili Coastal walisawazisha mabao yao kupitia kwa Yayo
Lutimba raia wa Uganda dakika 66 na Mkenya Ramadhani Salim 'Rama'
alifunga la pili dakika 81.
Mechi ya
pili dhidi ya Polisi Morogoro, Simba ndiyo ilianza kufunga bao lake
dakika ya 32 kupitia kwa Emmanuel Okwi raia wa Uganda lakini maafande
hao, walisawazisha bao hilo kipindi cha pili dakika ya 50 kupitia kwa
Danny Mrwanda matokeo yakawa 1-1.
Stendi
nayo iliwaotea Simba kwa staili hiyo hiyo wakatoa sare ya 1-1. Wekundu
hao wa Msimbazi walifunga bao lao dakika ya 35 kupitia kwa Shaaban
Kisiga na Stendi ilisawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Kheri Mohamed.
Phiri
aliwahi kukiri kuwa kikosi chake hicho kina tatizo la kucheza vizuri
kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili huwa hawafanyi vizuri, jambo
ambalo aliahidi kulitafutia ufumbuzi.
Ushindi
wa mechi tatu za Yanga walioupata kwa Tanzania Prisons matokeo yakawa
2-1, mabao yao yalifungwa dakika ya 18 na Andrey Coutinho na Simon Msuva
alifunga la pili dakika ya 70.
Matokeo
ya 2-1 walipoifunga JKT Ruvu, mabao yao yalifungwa dakika ya 35 na
Kelvin Yondani na Mnyarwanda Haruna Niyonzima alimalizia la pili dakika
ya 68
No comments:
Post a Comment