- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia jukwaani
YANGA
ilimsajili Emmanuel Okwi msimu uliopita kwa lengo la kuboresha fowadi
yake, lakini baadaye mchezaji huyo akatofautiana na timu hiyo na kufuata
taratibu za kisheria akarejea kwenye timu yake ya zamani, Simba ambayo
leo Jumamosi inacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Simba
wakafurahia ujio wa mchezaji huyo kwa vile anacheza kwa mapenzi zaidi
akiwa kwao, lakini wenzao wa Yanga bado wakawa na mawazo kutokana na
maneno ya mitaani pamoja na mamilioni ya shilingi ambayo Okwi alizoa
kiulaini.
Okwi
baada ya kukamilisha usajili wake Simba akawaambia Yanga akisema: "Yanga
msije uwanjani Oktoba 18." Kauli yake inamaanisha kwamba leo
atawadhalilisha.
Straika
Mbrazili Genilson Santos 'Jaja' aliposikia maneno yamezidi na watu
wanambeza akaipiga Azam mabao mawili kwenye mechi ya Ngao ya Jamii na
ilikuwa kama anawauliza mashabiki akisema: "Okwi wa kazi gani?"
Kama hiyo
haitoshi, Andrey Coutinho aliposikia makelele hayo akawaambia mashabiki
wa Yanga kwa ishara kwamba mambo yake yataonekana uwanjani hazungumzi
sana. Hayo ndiyo kati ya mambo yatakayonogesha mechi hiyo ambayo kila
upande umekoki silaha zake na kutamka kwamba 'No Retreat, No Surrender'
wakimaanisha kwamba 'Hakuna kujisalimisha wala kurudi nyuma' bali lazima
kieleweke ndani ya dakika 90.(T.K)
Yanga
yenye Wabrazili wanne akiwamo Kocha Mkuu, Marcio Maximo inakutana kwa
mara ya kwanza msimu huu na Simba ya kocha mwenye uwezo mkubwa wa kusoma
na kudhibiti mchezo, Mzambia Patrick Phiri.
Maximo na
Phiri wamewaambia mashabiki wa soka nchini waache nongwa, waelekee
uwanjani kushuhudia soka la aina yake ambalo halijawahi kuonekana tangu
msimu huu uanze.
YANGA
Mbali na
mazoezi mengine, Yanga imekuwa na siku tano za programu maalumu ya
maandalizi dhidi ya Simba ambazo zimekamilika jana Ijumaa.
Kikosi hicho kiliweka kambi eneo la Kunduchi katika hoteli ya Landamark na kufanyia mazoezi yake katika Uwanja wa Boko Veteran.
Kwa wiki
nzima, Maximo amekuwa akicheza na akili za wachezaji wake kwa kufanya
vikao visivyo rasmi ikiwa ni njia ya kuwatengeneza kisaikolojia, jambo
ambalo limekuwa likiongeza ufanisi na kupandisha morali kwa kikosi hicho
kilichoshika nafasi ya pili msimu uliopita.
Awali
viongozi pamoja na mashabiki wa Yanga walikumbwa na taharuki baada ya
nahodha wa timu, Nadir Haroub 'Cannavaro' kupata majeraha kwenye mechi
kati ya Taifa Stars na Benin, lakini kwa sasa ameonekana kuimarika hasa
baada ya kupata ruhusa ya kucheza kutoka kwa Daktari wa timu hiyo, Juma
Sufiani.
No comments:
Post a Comment