Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 9, 2014

BINGWA WA SPANEST CUP 2014 APATIKANA TARAFA YA PAWAGA NA IDODI


  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter




Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Leticia Warioba, kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Iringa, Dkt Christine Ishengoma, amehitimisha Mashindano
ya SPANEST CUP 2014 katika Tarafa ya Pawaga na Idodi yaliyoanza
kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi Julai 2014.
Mashindano hayo ambayo kauli mbiu yake ilikuwa ni PIGA VITA
UJANGILI, PIGA MPIRA, OKOA TEMBO yalishirikisha vijiji 21 kutoka
tarafa ya Idodi na Pawaga, vijiji ambavyo vinavyozunguka hifadhi ya
taifa ya Ruaha.
Katika mashindano hayo timu ya Itunundu kutoka Pawaga ndiyo
waliyoibuka washindi kwa ushindi mwembamba wa goli 1 dhidi ya timu
ya Kinyika ambayo ilikuwa tegemeo la wengi Tarafa ya Pawaga.
Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo Warioba aliwataka
viongozi kutenga maeneo kwa ajili ya kujenga viwanja vya vijana ili
kukuza na kuendeleza michezo mkoa wa Iringa.
Warioba alitoa Pongezi kwa mradi wa kulinda na kuhifadhi maeneo
yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania (SPANEST) kwa kuandaa
mashindano hayo kwa kushirikiana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, na
Chama cha mpira Wilaya ya Iringa.
Alisema kuwa Kampeni hiyo ni muhimu kwa kuwa imeweza kuwaweka
vijana na jamii kwa pamoja, katika jitihada za kutokomeza ujangili
kupitia michezo.
"Ni ukweli usiopingika kwamba Janga la ujangili limekithiri Tanzania,
hivyo hali hiyo kutishia kutokomea kwa wanyama hususani tembo
ambao ni urihi, fahari na sehemu kubwa ya uchumi wa Taifa letu,
pamoja na doria ambazo zimekuwa zikifanywa na vikosi maalumu lakini
mwitikio wa vijana bado umekuwa sio mzuri, hivyo kupitia mashindano
ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na SPANEST imekuwa ni njia
mwafaka ya kuwaleta karibu vijana kupitia elimu na hamasa katika vita
ya kupambana na ujangili" Alisema Warioba.
Hata hivyo Thamani ya Tembo mmoja anayeuwawa na majangili leo,
huliondolea taifa na jamii faida kubwa ambayo ingeweza kuendelea
kupatikana kupitia sekta ya utalii kwa hata zaidi ya miaka 70 ijayo
ambayo tembo anaweza kuishi.
Mapato yatokanayo na utalii katika hifadhi husaidia kutekeleza miradi
mbalimbali ya ujirani mwema ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa,
mabweni, Miradi ya maji na hifadhi ya mazingira .
Warioba alisema kuwa serikali itaendelea kuuunga mkono jitihada
zinazofanywa na SPANEST katika kukabiliana na vitendo vya ujangili
na jitihada za kuelimisha na kushirikisha jamii katika masuala ya
uhifadhi, utalii na pia kuhakikisha kuwa faida na manufaa ya
wanyamapori inawafikia wananchi hususani wale wanaoishi karibu na
maeneo yaliyohifadhiwa.
Naye Mkurugenzi wa mipangio na miradi ya maendeleo Tanapa, Dkt
Ezekiel dembe,alisema kuwa anaamini siku moja Pawaga na Idodi
watashiriki ligi kuu hivyo kuna kila sababu yakuendeleza vipaji hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa sheria, utawala na
wanachama (TFF), Eliud Mvela akimuwakilisha rais wa (TFF), Jamali
Malinzi alisema kuwa mashindano hayo yameingia kwenye ratiba ya
TFF, hivyo ameahidi kushirikiana na SPANEST ili kuboresha
mashindano hayo.
Sawia na hayo amechangia mipira 5 kwa ajili ya kuimarisha na
kuboresha zawadi kwa washindi wa SPANEST CUP 2014.
Naye Mratibu wa mradi wa kulinda na kuhifadhi maeneo
yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania, Godwell Ole Meing'ataki
aliwaomba wananchi kutoa taarifa za usahihi kwenye namba
0800751212 iliyozinduliwa na mgeni rasmi baada ya kukabidhi zawadi
kwa washindi wa SPANEST CUP 2014.Huku akisema kuwa taarifa zote
hizo watakazotoa wananchi zitakuwa za siri.
Meing'ataki alisema vijana wengi hukamatwa na kufungwa kwa kuwa
ndio ambao wanahusika na ujangili, hivyo alitoa wito kwa vijana zaidi
ya 150,000 waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo kuacha
kutumiwa kwenye ujangili kwani jambo hilo limekuwa likiathiri familia
zao pale wanapofungwa.
Aliwaahidi wakazi wa Pawaga na Idodi kuwa mashindano hayo
yataendelea kufanyika kila mwaka ili kuokoa tembo ambao idadi kubwa
ya ujangili imeanza kupungua ukilinganisha na takwimu za mwaka jana.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ambaye ni timu ya
Itunundu kutoka Tarafa ya Pawaga amepata; Kikombe, Medali ya
Dhahabu, Jezi seti moja, mipira mitatu, Cheti, na Fedha shilingi
300,000/=, Kutembelea hifadhi ya Ruaha na kulala siku moja hifazini,
kucheza mechi ya kirafiki wakiwa Ruaha.
Kwa upande wa timu ya Kinyika ambayo imeshika nafasi ya pili imepata
Medani ya Fedha shilingi 200,000/=, Mipira 2, pamoja na Cheti.
Timu ya Kitisi kutoka Tarafa ya Idodi imejinyakulia Fedha taslimu
shilingi 100,000/= , Medani ya Shaba na Cheti kwa kuwa nafasi ua tatu.
Pia timu ya Kitisi ilipata zawadi ya shilingi 100,000 kwa kuonyesha
nidhamu mwanzo hadi mwisho wa mashindano hayo.
Kwa upande wake mfungaji bora ambaye ni Siani Mkadange, kutoka
timu ya itunundu Tarafa ya Pawaga, alijipatia shilingi 100,000/=.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG