Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 9, 2014

SAA LA 25- riwaya inayogusa maisha yako... SAA LA 25 Ilipoishia... Haikuchukua muda tax ilifika mahali panapotakiwa. Zai alilipana kulijongea geti kubwa la nyumba hiyo. Baada ya kubofya kengele mlango ulifunguka wenyewe nae akaingia ndani, hakuwa mgeni na nyumba hiyo ambayo amekwishafika mara kadhaa, moja kwa moja alipitiliza sebuleni na kulakiwa na mwenyeji wake Mr Dam Dam. Wakiwa juu ya kochi kubwa lililo sebuleni hapo makumbatiano hayakuwa haba na mabusu motomoto kabla hawajakokotana chumbani. “Darlin, nina shida mwenzio” zai alianza ubembe wake kwa mwanaume huyo “Sema, nakusikiliza darling, hakuna shida itakayokuwa ngumu mbele ya pesa.” Zai alimueleza Dam Dam mambo yote juu ya Kautipe kuwekwa ndani kwa kosa la kushukiwa kuwa na biashara ya bangi, lakini kila alipotaka kumjuza kuhusu Ashura roho yake ilisitasita. “Ok, nimekuelewa, sasa siku ya kesi wewe utamuwekea dhamana ya shilingi milioni moja, sawa?” Damdam alimueleza Zai huku akimchezea chuchu zake zilizochongoka kama mshale. Zai aliitika kwa kichwa akaona kuwa hapo moja amelimaliza na linalobaki endelea... “Ok, nimekuelewa, sasa siku ya kesi wewe utamuwekea dhamana ya shilingi milioni moja, sawa?” Damdam alimueleza Zai huku akimchezea chuchu zake zilizochongoka kama mshale. Zai aliitika kwa kichwa akaona kuwa hapo moja amelimaliza na linalobaki angemshirikisha mwingine kumsaidia. “Nashukuru Damdam.” Zai alimshukuru mwanaume huyo na kumkumbatia, bila kusita Damdam naye alimkumbatia Zai kwa bashasha kubwa na mapenzi yao yamuda mfupi kuchukua nafasi yake juu ya kochi hilo kubwa huku wakisindikizwa kwa muziki laini uliotoka kwenye spika kubwa za kisasa ambazo Damdam alizinunua alipokuwa katika moja ya safari zake huko Uchina. € € € € “Mgonjwa wenu hali yake si nzuri, amepooza mwili, hivyo hana uwezo wa kufanya lolote kwa nguvu zake” Dakta Msola aliwaeleza ndugu wa mzee Njiku, walipokuja kumtazama hospitalini hapo. Sura za huzuni zilitawala nyuso za ndugu hawa walitazamana kwa muda bila kupata chochote cha kuongea. “Kwa vyovyote wamemloga” Dada wa Mzee Njiku alianza kubwabwaja kama kawaida yake huku akitoka nje ya chumba cha daktari kilichopo katika wodi hiyo. “Hivi wewe kwa nini unapenda kuamini uchawi?” kaka yake alimuuliza kwa hasira. “Mimi najua, wamemloga kaka yangu” aliendelea kusisitiza kaui yake “Sasa wewe mwema kwako nani?” kakaye aliuliza tena “Hamna mwema, wote wachawi tu. Yule mkewe wa kwanza alimloga kulipiza kisasi, na huyu nae mchawi sasa anataka kurithi mali, na hazipati”, aling’aka dada yule huku akirusharusha mikono yake kwa hasira. “Jamani ndugu yetu ndiyo huyo, tunamsaidiaje? Maana sasa hana hata pa kuishi” ndugu wa mzee Njiku walikusanyika kuzungumza machache juu ya mgonjwa wao. Kila mtu alikuwa mzito kutoa maamuzi ya nini cha kufanya, nani amchukue kumtunza, kila mmoja alijesemea moyoni ‘nani abebe mzigo huo’. Baada ya mawili matatu kuzungumzwa waliafikiana kumsafirisha nyumbani kijijini. Wakiwa katika mazungumzo hayo gari ya mama Minja ilisimama taratibu mbele ya jengo hilo la hospitali, mama Njiku, mke wa ndoa wa mzee Njiku aliteremka na moja kwa moja akamuendea shemeji yake. “Asante kwa ujumbe, niliupata ila nilikuwa mbali, namuomba mume wangu niondoke nae, nitamtunza mwenyewe, huyu ni mume wangu” mama Njiku alisema maneno hayo ambayo yalimgusa kila mmoja wao, wakikumbuka walivyomwita mchawi, walivyomfukuza kama mbwa na kumthamini mwanamke mwengine ambaye sasa wameona yaliyompata kaka yao. Kaka wa mzee Njiku alimwita pembeni mama Njiku na kumueleza majibu yote ya daktari bila kumficha. Mama Njiku aliyapokea majibu hayo na moja kwa moja alimuendea daktari kwa mazungumzo ya kina. “Licha ya kupooza, mumeo ameathirika na gonjwa la ukimwi, hivyo nizuri hata wewe kufanya vipimo kwa uhakika zaidi”, Mama Njiku hakuonekana kushtuka kwa jambo hilo kwani alilitegemea muda wowote kutokea, alitulia kimya akiwa kajishika tama, mawazo yake yalimrudisha nyuma kabisa enzi za wawili hao wakiwa katika mtafaruku mzito… “Sawa, mi ntaondoka ntakuacha, lakini kumbuka maradhi mume wangu, hao unaowathamini leo hujui wangapi walifanywa hivyo” Mama Njiku alikuwa akiongea huku akitoa machozi akimueleza kwa uchungu baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa mumewe… …aligutuka aliposikia mlio wa chupa ya dawa iliyoanguka kwa bahati mbaya na kupasuka. Mama Njiku alikubali kufanya vipimo ili kuhakikisha afya yake, baada ya majibu kutoka aligundulika hakuwa na maambukizi. Alinyanyuka kutoka katika meza ile na kuingia wodini kumuona mumewe. Aliketi pembeni kabisa ya Mzee Njiku walitazamana uso kwa uso, machozi yaliwalenga wote wawili kila mmoja alijikuta ana haki ya kumsamehe mwingine. Mzee Njiku hakuwa na uwezo hata wa kuongea kutokana na hali yake, moyoni alitamani atamke japo neon moja la msamaha kwa mkewe lakini haikuwa hivyo, aliongea ndani ya moyo wake Nisamehe mke wangu Yote ni makosa yangu Ulifungwa moyo wangu Sikujua nifanyalo Niombee kwa wanangu Sahau kauli zangu ‘mefika safari yangu Ya kuuacha ulimwengu Enyi waume wenzangu Jifunzeni toka kwangu Niliivunja nyumba yangu Mapenzi yalihadaa Jihadhari na rafiki Wengi wao wanafiki Wabilah tawfiq Watakupoteza hakika Moyo wangu waniuma Kwa niloyafanya nyuma Sina mbele wala nyuma Kitandani naishia Ninatubu kwa Mungu Na kwako mke wangu Ndugu na watoto wangu Goti ninawapigia Mama Njiku alizidi kulia huku akiwa ameushika mkono wa mume wake ambaye sasa hakuweza kufanya lolote, Mama Njiku aliyahisi maneno hayo kutoka kwenye macho ya mumewe, aliuhisi msamaha wa nguvu na maneno mazito yaliyougusa moyo wake. Alipiga magoti sakafuni na kumtazama mumewe aliye kufani kwa ukaribu zaidi, kinywa chake kilifunguka akasema Laazizi mume wangu U mweupe moyo wangu Hakuna kinyongo kwangu Mimi nimekusamehe Dunia yetu mapito Mambo mpwitompwito Hilo nalo ni pito Mimi nimekusamehe Marefu pa si na ncha Hamna kutwa kwa kucha Maadam kumekucha Mimi nimekusamehe Najua unaumia Kwa yote yalotukia Ni njia ya kupitia Mimi nimekusamehe Siku zote nilijua Kuwa kwangu utarudia Mimi ni mke wandoa Wengine viruka njia Mateso nilipitia Gerezani kuingia Maisha kunichachia Kila kitu kupoteza Yote tumuachie Mungu Muumba nchi na mbingu Toka kwako na kwangu Maombi tumtolee Nakupenda mume wangu Kuliko wazazi wangu Narudisha moyo wangu Kwako laaziz wangu. Mama Njiku aliuinua mkono wa mumewe na kuubusu kisha kuukumbatia na kulia kwa machozi ya upendo. Masikini, mzee Njiku, muda wake ulikuwa umefika tamati, macho yake yalishindana na kiza kinene lakini nuru ilizidi kufifia kwa haraka, alihisi mabadiliko ya maisha yakiivamia roho yake, mara tu, roho yake ikaacha mwili, macho yakafumba akapumzika kwa amani. Mama Njiku alibubujikwa na machozi, alilia kwa uchungu, alitamani mumewe arudi wamalizie maisha lakini haikuwa hivyo, mauti yalikwishamfika. € € € € Kautipe alitulia kimya katika chumba cha mahabusu pale mahakama ya mwanzo ya Chang’ombe. Alijua wazi kuwa mwisho wake umefika kwa kosa lisilomhusu, atafungwa pasipo kutarajia. Jalada lake lilifika, kizimbani akasimama pamoja na Rasta, mahakama ikaendelea hakukuwa na utetezi, hakimu alipoitisha dhamana kama ipo, Kautipe hakuamini macho yake. Zai alijitokeza na kumuwekea dhamana Kautipe. Mambo yote ya kimahakama yalipomalizika Kautipe na Zai walitoka mahakamani na kuketi kwenye grosary moja iliyopo katika eneo hilo, waliagiza vinywaji na kunywa taratibu. “Pole mdogo wangu!” Zai alianzisha mazungumzo “Asante da Zai, mi nimekamatwa bure tu” Kautipe aliongea huku analia “Basi yataisha tu maadamu upo nje, tutafanya kinachowezekana” Zai alimfaraiji mwenzake. “Nitashukuru, mi naogopa” Kautipe aliendelea kulia “Usiogope we tulia tu”. Punde si punde gari moja nyeusi salon ilisimama eneo hilo, kioo cha mbele upande wa kulia kiliteremka taratibu, hakuwa mwingine bali Mr Damdam. Zai alijiinua na Kautipe wote wakaingia garini. Msichana mmoja alievalia baibui alikuwa akifuatilia nyendo zote za Zai na Kautipe kila hatua mapka walipoingia garini humo, mara tu walipoondoka na ye alichuku tax kuwafuata. “Fuata hiyo gari mpaka itapoishia” alimuamuru dereva, na dereva alitii amri ya mteja wake.

SAA LA 25
 Ilipoishia...

 
Haikuchukua muda tax ilifika mahali panapotakiwa. Zai alilipana kulijongea geti kubwa la nyumba hiyo. Baada ya kubofya kengele mlango ulifunguka wenyewe nae akaingia ndani, hakuwa mgeni na nyumba hiyo ambayo amekwishafika mara kadhaa, moja kwa moja alipitiliza sebuleni na kulakiwa na mwenyeji wake Mr Dam Dam. Wakiwa juu ya kochi kubwa lililo sebuleni hapo makumbatiano hayakuwa haba na mabusu motomoto kabla hawajakokotana chumbani.
Darlin, nina shida mwenzio” zai alianza ubembe wake kwa mwanaume huyo
“Sema, nakusikiliza darling, hakuna shida itakayokuwa ngumu mbele ya pesa.” Zai alimueleza Dam Dam mambo yote juu ya Kautipe kuwekwa ndani kwa kosa la kushukiwa kuwa na biashara ya bangi, lakini kila alipotaka kumjuza kuhusu Ashura roho yake ilisitasita.
“Ok, nimekuelewa, sasa siku ya kesi wewe utamuwekea dhamana ya shilingi milioni moja, sawa?” Damdam alimueleza Zai huku akimchezea chuchu zake zilizochongoka kama mshale. Zai aliitika kwa kichwa akaona kuwa hapo moja amelimaliza na linalobaki 

endelea...


“Ok, nimekuelewa, sasa siku ya kesi wewe utamuwekea dhamana ya shilingi milioni moja, sawa?” Damdam alimueleza Zai huku akimchezea chuchu zake zilizochongoka kama mshale. Zai aliitika kwa kichwa akaona kuwa hapo moja amelimaliza na linalobaki angemshirikisha mwingine kumsaidia.
“Nashukuru Damdam.” Zai alimshukuru mwanaume huyo na kumkumbatia, bila kusita Damdam naye alimkumbatia Zai kwa bashasha kubwa na mapenzi yao yamuda mfupi kuchukua nafasi yake juu ya kochi hilo kubwa huku wakisindikizwa kwa muziki laini uliotoka kwenye spika kubwa za kisasa ambazo Damdam alizinunua alipokuwa katika moja ya safari zake huko Uchina.
€ € € €
“Mgonjwa wenu hali yake si nzuri, amepooza mwili, hivyo hana uwezo wa kufanya lolote kwa nguvu zake” Dakta Msola aliwaeleza ndugu wa mzee Njiku, walipokuja kumtazama hospitalini hapo. Sura za huzuni zilitawala nyuso za ndugu hawa walitazamana kwa muda bila kupata chochote cha kuongea.
“Kwa vyovyote wamemloga” Dada wa Mzee Njiku alianza kubwabwaja kama kawaida yake huku akitoka nje ya chumba cha daktari kilichopo katika wodi hiyo.
“Hivi wewe kwa nini unapenda kuamini uchawi?” kaka yake alimuuliza kwa hasira.
“Mimi najua, wamemloga kaka yangu” aliendelea kusisitiza kaui yake
“Sasa wewe mwema kwako nani?” kakaye aliuliza tena
“Hamna mwema, wote wachawi tu. Yule mkewe wa kwanza alimloga kulipiza kisasi, na huyu nae mchawi sasa anataka kurithi mali, na hazipati”, aling’aka dada yule huku akirusharusha mikono yake kwa hasira.
“Jamani ndugu yetu ndiyo huyo, tunamsaidiaje? Maana sasa hana hata pa kuishi” ndugu wa mzee Njiku walikusanyika kuzungumza machache juu ya mgonjwa wao. Kila mtu alikuwa mzito kutoa maamuzi ya nini cha kufanya, nani amchukue kumtunza, kila mmoja alijesemea moyoni ‘nani abebe mzigo huo’. Baada ya mawili matatu kuzungumzwa waliafikiana kumsafirisha nyumbani kijijini.
Wakiwa katika mazungumzo hayo gari ya mama Minja ilisimama taratibu mbele ya jengo hilo la hospitali, mama Njiku, mke wa ndoa wa mzee Njiku aliteremka na moja kwa moja akamuendea shemeji yake.
“Asante kwa ujumbe, niliupata ila nilikuwa mbali, namuomba mume wangu niondoke nae, nitamtunza mwenyewe, huyu ni mume wangu” mama Njiku alisema maneno hayo ambayo yalimgusa kila mmoja wao, wakikumbuka walivyomwita mchawi, walivyomfukuza kama mbwa na kumthamini mwanamke mwengine ambaye sasa wameona yaliyompata kaka yao. Kaka wa mzee Njiku alimwita pembeni mama Njiku na kumueleza majibu yote ya daktari bila kumficha. Mama Njiku aliyapokea majibu hayo na moja kwa moja alimuendea daktari kwa mazungumzo ya kina.
“Licha ya kupooza, mumeo ameathirika na gonjwa la ukimwi, hivyo nizuri hata wewe kufanya vipimo kwa uhakika zaidi”, Mama Njiku hakuonekana kushtuka kwa jambo hilo kwani alilitegemea muda wowote kutokea, alitulia kimya akiwa kajishika tama, mawazo yake yalimrudisha nyuma kabisa enzi za wawili hao wakiwa katika mtafaruku mzito…
“Sawa, mi ntaondoka ntakuacha, lakini kumbuka maradhi mume wangu, hao unaowathamini leo hujui wangapi walifanywa hivyo” Mama Njiku alikuwa akiongea huku akitoa machozi akimueleza kwa uchungu baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa mumewe…
…aligutuka aliposikia mlio wa chupa ya dawa iliyoanguka kwa bahati mbaya na kupasuka. Mama Njiku alikubali kufanya vipimo ili kuhakikisha afya yake, baada ya majibu kutoka aligundulika hakuwa na maambukizi. Alinyanyuka kutoka katika meza ile na kuingia wodini kumuona mumewe. Aliketi pembeni kabisa ya Mzee Njiku walitazamana uso kwa uso, machozi yaliwalenga wote wawili kila mmoja alijikuta ana haki ya kumsamehe mwingine. Mzee Njiku hakuwa na uwezo hata wa kuongea kutokana na hali yake, moyoni alitamani atamke japo neon moja la msamaha kwa mkewe lakini haikuwa hivyo, aliongea ndani ya moyo wake
Nisamehe mke wangu
Yote ni makosa yangu
Ulifungwa moyo wangu
Sikujua nifanyalo
Niombee kwa wanangu
Sahau kauli zangu
‘mefika safari yangu
Ya kuuacha ulimwengu
Enyi waume wenzangu
Jifunzeni toka kwangu
Niliivunja nyumba yangu
Mapenzi yalihadaa
Jihadhari na rafiki
Wengi wao wanafiki
Wabilah tawfiq
Watakupoteza hakika
Moyo wangu waniuma
Kwa niloyafanya nyuma
Sina mbele wala nyuma
Kitandani naishia
Ninatubu kwa Mungu
Na kwako mke wangu
Ndugu na watoto wangu
Goti ninawapigia
Mama Njiku alizidi kulia huku akiwa ameushika mkono wa mume wake ambaye sasa hakuweza kufanya lolote, Mama Njiku aliyahisi maneno hayo kutoka kwenye macho ya mumewe, aliuhisi msamaha wa nguvu na maneno mazito yaliyougusa moyo wake. Alipiga magoti sakafuni na kumtazama mumewe aliye kufani kwa ukaribu zaidi, kinywa chake kilifunguka akasema
Laazizi mume wangu
U mweupe moyo wangu
Hakuna kinyongo kwangu
Mimi nimekusamehe
Dunia yetu mapito
Mambo mpwitompwito
Hilo nalo ni pito
Mimi nimekusamehe
Marefu pa si na ncha
Hamna kutwa kwa kucha
Maadam kumekucha
Mimi nimekusamehe
Najua unaumia
Kwa yote yalotukia
Ni njia ya kupitia
Mimi nimekusamehe
Siku zote nilijua
Kuwa kwangu utarudia
Mimi ni mke wandoa
Wengine viruka njia
Mateso nilipitia
Gerezani kuingia
Maisha kunichachia
Kila kitu kupoteza
Yote tumuachie Mungu
Muumba nchi na mbingu
Toka kwako na kwangu
Maombi tumtolee
Nakupenda mume wangu
Kuliko wazazi wangu
Narudisha moyo wangu
Kwako laaziz wangu.
Mama Njiku aliuinua mkono wa mumewe na kuubusu kisha kuukumbatia na kulia kwa machozi ya upendo. Masikini, mzee Njiku, muda wake ulikuwa umefika tamati, macho yake yalishindana na kiza kinene lakini nuru ilizidi kufifia kwa haraka, alihisi mabadiliko ya maisha yakiivamia roho yake, mara tu, roho yake ikaacha mwili, macho yakafumba akapumzika kwa amani.
Mama Njiku alibubujikwa na machozi, alilia kwa uchungu, alitamani mumewe arudi wamalizie maisha lakini haikuwa hivyo, mauti yalikwishamfika.
€ € € €
Kautipe alitulia kimya katika chumba cha mahabusu pale mahakama ya mwanzo ya Chang’ombe. Alijua wazi kuwa mwisho wake umefika kwa kosa lisilomhusu, atafungwa pasipo kutarajia.
Jalada lake lilifika, kizimbani akasimama pamoja na Rasta, mahakama ikaendelea hakukuwa na utetezi, hakimu alipoitisha dhamana kama ipo, Kautipe hakuamini macho yake. Zai alijitokeza na kumuwekea dhamana Kautipe. Mambo yote ya kimahakama yalipomalizika Kautipe na Zai walitoka mahakamani na kuketi kwenye grosary moja iliyopo katika eneo hilo, waliagiza vinywaji na kunywa taratibu.
“Pole mdogo wangu!” Zai alianzisha mazungumzo
“Asante da Zai, mi nimekamatwa bure tu” Kautipe aliongea huku analia
“Basi yataisha tu maadamu upo nje, tutafanya kinachowezekana” Zai alimfaraiji mwenzake.
“Nitashukuru, mi naogopa” Kautipe aliendelea kulia
“Usiogope we tulia tu”.
Punde si punde gari moja nyeusi salon ilisimama eneo hilo, kioo cha mbele upande wa kulia kiliteremka taratibu, hakuwa mwingine bali Mr Damdam. Zai alijiinua na Kautipe wote wakaingia garini.
Msichana mmoja alievalia baibui alikuwa akifuatilia nyendo zote za Zai na Kautipe kila hatua mapka walipoingia garini humo, mara tu walipoondoka na ye alichuku tax kuwafuata.
“Fuata hiyo gari mpaka itapoishia” alimuamuru dereva, na dereva alitii amri ya mteja wake.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG