- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Kocha Jose Mourinho kulia akimpongeza Nemanja Matic baada ya kufunga bao pekee la ushindi usiku huu
CHELSEA
imepata ushindi wa ugenini katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya
kuifunga Sporting Lisbon ya Ureno bao 1-0, wakati Manchester City
imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Roma ya Italia usiku huu.
Katika
mchezo wa Kundi G, bao la Nemanja Matic dakika ya 34 limemfanya kocha
Jose Mourinho aitambie timu ya nchini kwake, Sporting.
Fernandinho wa Manchester City (kushoto) akigombea mpira na Radja Nianggolan wa AS Roma (kulia)
Uwanja wa
Etihad, Sergio Aguero alitangulia kuifungia City kwa penalti dakika ya
nne kabla ya mkongwe Francesco Totti kuisawazishia Roma dakika ya 23
katika mchezo wa Kundi E.
Bao pekee
la Thomas Mueller dakika ya 22 limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0
ugenini dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika mchezo mwingine wa Kundi E.
mchezo mwingine wa kundi hilo usiku huu, Schalke 04 imelazimishwa sare
ya 1-1 nyumbani na Maribor.(T.K)
Mchezo mwingine wa Kundi hilo, APOEL Nicosia imelazimishwa sare ya 1-1 na Ajax nyumbani bao la wenyeji likifungwa na Manduca dakika ya 31 na la wageni likifungwa na Lucas Anderson mapema dakika ya 28.
Kundi H, BATE Borisov imeichapa 2-1 Athletic Bilbao nyumbani mabao ya washindi yakifungwa na Denis Polyakov dakika ya 19 na Karnitskiy dakika ya 41, wakati bao la wageni lilifungwa na Aritz Aduriz dakika ya 45.
Shakhtar Donetsk imelazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na FC Porto, mabao ya wenyeji yakifungwa na Alex Teixeira dakika ya 52 na Luiz Adriano dakika ya 85, wakati ya wageni yote yamefungwa na Jackson Martinez dakika ya 89 kwa penalti na 90.
MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA JANA USIKU
Kundi E
CSKA Moscow 0-1 Bayern Munich
Manchester City 1-1 AS Roma
Kundi F
APOEL Nicosia 1-1 Ajax
PSG 3-2 Barcelona
Kundi G
Schalke 04 1-1 Maribor
Sporting 0-1 Chelsea
Kundi H
BATE Borisov 2-1 Athletic Bilbao
Shakhtar Donetsk 2-1 FC Porto
No comments:
Post a Comment