Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, October 1, 2014

Waliodhurika kwa togwa Songea sasa wafikia watu 340




Idadi ya watu waliolazwa hospitalini kwa kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu katika 
Kijiji cha Litapwasi, Kata ya Mpitimbi mkoani Ruvuma imeongezeka kutoka 270 hadi 340.
Tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya watu kushiriki sherehe ya Kipaimara ambako walikula, 
kunywa pombe na togwa na baadaye wale waliokunywa togwa walianza kuumwa matumbo, 
kuhara na kutapika.
Hadi jana, watu 102 walikuwa bado wamelazwa katika Zahanati ya Lyangweni, Hospitali ya 
St. Joseph Peramiho na Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.
Tayari watu watano wanashikiliwa na Polisi kwa upelelezi kuhusiana na tukio hilo, 

akiwamo Baba Mzazi wa mtoto Dickson aliyepata kipaimara, Enes Nungu (47).(T.K)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Mskhiela aliwataja watu wengine 
wanaoshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Songea kwa mahojiano kuwa ni 
Benedict Nungu (76), Esebius Komba (36), Sadiki Masodi (65) na John 
Kaulangudidi. Mtu anayedaiwa kukabidhiwa ufunguo chumba cha vinywaji kabla 
ya kugawiwa kwa wananchi, Ridhiwani Shawa haijulikani alipo.
Mabaki ya chakula, togwa na pombe ya kienyeji vilichukuliwa juzi na kupelekwa 
kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi.
Kamanda Mskhiela alitoa wito kwa wananchi wanaoandaa sherehe kuhakikisha 
wanafanya hivyo katika mazingira mazuri na yenye usalama ili kuepuka athari kama hizo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Peramiho, Dk Vanace Mushi alisema hadi 
jana, watu waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo walikuwa 34 na hakukuwa 
na mgonjwa aliyeruhusiwa kurudi nyumbani.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Majuto Mlawa 
alisema wagonjwa tisa wa rufaa walipokewa na kupatiwa matibabu huku hali zao 
zikiwa mbaya.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu alisema:
 "Jambo hili limenisikitisha sana, nimeumizwa sana nawapa pole wote 
waliopatwa na tatizo hilo naamini Mwenyezi Mungu atawasaidia na watapona 
na kurejea katika hali zao za kawaida."
Hata hivyo, Mwambungu alisema hiyo ni ajali kama nyingine, hivyo anaviachia 
vyombo vya usalama na wataalamu wa afya kupata ukweli. Pia aliwataka 
wananchi kuwa makini pindi wanapoandaa vyakula na pombe za kienyeji katika 
sherehe mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG