Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, October 13, 2014

Gaza yaahidiwa mamilioni

  • Written by Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 
John Kerry
Wafadhili katika mkutano unaoendelea mjini Cairo wameahidi kutoa dola za kimarekani bilioni tano nukta nne kwa ajili ya Gaza, nusu ya fedha hiyo ni kwa ajili ya ukarabati kutokana na uharibifu uliofanywa kwa takriban siku 50 za vita na Israel mapema mwaka huu.
Jumla ya kiasi hicho cha fedha kilichotangazwa na Waziri wa mambo ya nje wa Norway Borge Brende ni zaidi ya mabilioni ya dola ya kiasi ambacho Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas alikiomba.
Nchi ya Qatar pekee imeahidi kutoa dola bilioni moja. Akizungumza katika mji mkuu wa Misri Cairo, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry huu ni muda wa kusimika mpango wa muda mrefu wa amani.
Tamko hilo la waziri wa mambo ya nje wa Norway Borge Brende ni zaidi ya dola bilioni ya zile ambazo raisi Mahmoud Abbas aliziomba.
nchi ya Qatar pekee imeahidi kutoa dola bilioni moja. Akizungumza katika mji mkuu wa Misri,Cairo katibu mkuu wa Ikulu ya Marekani John Kery amesema huu ni wakati sasa wa kusimika mpango wa muda mrefu wa amani ,ili kuhakikisha heshima ya wapalestina na usalama wa Israel umeimarishwa.Na akaongeza kuwa ili kufikia malengo hayo hakuna budi mabadiliko makubwa yafanyike kwanza.
Muda wa usitishwaji mapigano ndio njia mbadala kwa Israel na heshima kubwa kwa Wapelestina. Hakuna njia yoyote zaidi ya kuwaridhisha kila upande kwa madai yao.hatua zaidi za makusudi za kusitisha vita ama usalama wa Israel ama haki kwa wapalestina huko Gaza.
hahakuna njia nyingine ya kuwaridhisha ikiwa mwafaka hautafikiwa na mwishowe kuweka mpango wa muda mrefu wa amani na kuwajengea uwezo wa majaaliwa ya siku za baadaye.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG