Manchester City
Mechi za kombe la ligi ya CAPITALA ONE CUP zimeendelea usiku wa kuamkia leo viwanjani.
Manchester
City ikicheza nyumbani ilijikuta ikiwaduwaza mashabiki wake baada ya
kukubali kichapo cha mabao 2 bila majibu kutoka kwa Newcastle utd na
kutupwa nje kabisa ya mashindano hayo.Nayo Tottenham hotspurs iliutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichabanga vilivyo kabisa Brighton kwa jumla ya mabao 2-0.
Nayo Southampton ikairarua Stoke City kwa jumla ya mabao 3-2.
Kwa matokeo haya ya sasa, katika robo fainali Chelsea watapambana na Derby, wakati Tottenham watavaana na Newcastle utd. Nayo Liverpool itapepetana na Bournemouth


No comments:
Post a Comment