Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, October 17, 2014

NILIVYOKATAA RUSHWA YA WACHAWI NA KUWA ADUI YAO-12

ILIPOISHIA:
Siku zilikatika huku biashara zangu zikiendelea na mipango ya harusi yangu ikianza taratibu kwa kumshirikisha mama mzazi kwa vile mama mdogo aligeuka udui yangu mkubwa, aliapa kutonisamehe  hata nikifa haniziki akifa nisimzike. Nilijiuliza kosa kubwa lilikuwa nini kiasi cha kujenga uadui mkubwa kama huo kama ubaya alinifanyia yeye lakini ajabu ndiye anayenichukia kama shetani.
Ajabu nyingine ambayo ilikuwa haijapata dawa nilikuja kuigundua baadaye, tatizo la ndoa yangu kuchelewa. SASA ENDELEA...
Kila mzazi mwenzangu alipojiandaa tufunge ndoa, aliyumba kiuchumi au kuwa mlevi sana kitu ambacho mwanzo sikukijua.  Kila alivyojipanga kwa ajili ya harusi hali ilikuwa mbaya, kuna kipindi ilibidi nimsaidie pesa za matumizi toka kwenye biashara zangu kutokana na mambo yake kwenda kombo.
Wakati huo hata biashara zangu zilianza kuyumba, nilikuwa nauza ndoo sita zikaanza kushuka mpaka zikawa tatu. Hali ile mwanzoni sikuielewa kwa kuamini huenda ni hali ya biashara. Nami sikukaa kimya nilihangaika mpaka kuweza kufikisha ndoo nne na nusu.
Mtoto wa kike pamoja na udogo wangu lakini vita nilipambana vilivyo. Niliamini roho ziliwauma kuonekana nashindana  na watu wazima japokuwa aliamini nilichelewa kuliona jua kama alivyosema lakini nilimtoa jasho la kwapa mama mtu mzima. Lakini bado aliapa kunitia adabu kwa vile nataka kutunishiana msuli na mtu aliyenisafisha haja zangu nilipokuwa mdogo.
KURUDI KWA MJOMBA KUTOKA MAREKANI
Tukiwa bado tupo  katika msigano mkali na mama mdogo, mjomba wangu, mdogo wake mama aliyekuwa akiishi Marekani alirudi Tanzania. Kwetu ilikuwa furaha kubwa kwa vile siku za nyuma aliporudi kila mmoja alipatiwa anachokitaka hivyo kila ujio wake familia yote ilifurahi.
Wakati huo alikuwa amerudi moja kwa moja tofauti na mwanzo alipokuja likizo na kuondoka. Aliporudi aliikuta hali ya msigano mkali ndani ya nyumba kila mtu kivyake. Mwanzo hakusema kitu alifuatilia kwa kuuliza tatizo nini, nilimwelezea kama lilivyotokea kwa mimi kujifanya sijui lolote.
Hakupendezwa na hali ile ya kuishi nyumba moja  kila mtu kivyake. Hivyo alichukua jukumu la kutupatanisha, tuliitwa ili tulizungumze tumalize tofauti zetu. Kwa upande wangu nilikuwa tayari kusamehe kwa vile sikuwahi kufikiria kumfanyia ubaya ma’mdogo hata siku moja.
Mjomba alituomba tumalize tofauti zetu, lakini mama mdogo alisema hawezi kunisamehe mpaka anaingia kaburini.
“Nasema hivi, sitamsamehe huyu shetani mtoto, mdogo wa umbile lakini mwanga mkubwa. Tunakaa nyumba moja na mchawi, ndiyo maana wanangu hawaolewi kwa ubaya wa mtoto huyu.  Amekuwa akitutia aibu mtaani kwa mambo yake ya ushirikina kwenye biashara zake, nani hajui kuwa anafanya biashara kichawi,” mama mdogo alisema mpaka povu likamtoka mdomoni.
“Dada tunachokizungumza hapa ni kumaliza tofauti na mwanao si masuala mengine.”
“Nimesema hivi sina suluhu na shetani huyu, nataka ahame nyumba hii.”
“Lakini dad...”
“Hakuna cha lakini, nyumba hii lazima aondoke mmoja mimi ama yeye, kama nitashindwa kumtoa basi nitaondoka mimi.”
Muda wote nilikaa kimya kuogopa kufunua mdomo wangu kwa kuhofia kuchafua hali ya hewa kwa vile hata mimi lilinifika kooni kwa shutuma za uongo za kunichafua wakati kila kitu alikuwa akikijua na mchawi alikuwa mwenyewe. Mjomba alishindwa kutuweka pamoja.
Baada ya mjomba kushindwa  kusuluhisha alituacha kila mtu na maisha yake. Mama mdogo naye alisimamia msimamo wake wa kutaka mimi nihame pale, moyoni nilijisemea atahama yeye kwa vile alielewa kama kizingiti asiyejishughulisha na kitu chochote na kuendekeza ushirikina.
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, ghafla mjomba naye akaungana na dada yake kunitaka nihame nikapange sehemu nyingine ili niepushe shari.
“Mjomba unasema nikapange ili niepushe shari, gharama za nyumba utanilipia?”
“Atakulipia mzazi mwenzio, aliweza vipi kukarabati nyumba si yake ashindwe kukupangia chumba.”
“Mjomba siwezi kuhama kwa vile siwezi kuingia gharama mara mbili.”
“Gharama mara mbili kivipi?”
“Wewe mwenyewe ulipoondoka unajua nyumba ilivyokuwa na umerudi umeona mabadiliko makubwa. Nina imani bibi amekwambia nani aliyefanya hivi na amefanya kwa ajili ya nani kama siyo mimi mzazi mwenzie. Hivyo siwezi kuhama labda mrudishe gharama zetu.”
“Sawa, lakini uadui uliopo ni mbaya sana mnaweza kutiliana hata sumu.”
“Mjomba, mi sina ubaya na mama mdogo kwa vile sijawahi kumdharau wala kumfanyia kitu kibaya nashangaa hizo tuhuma zimetoka wapi.”
“Sawa lakini heri ukae mbali na shari.”
“Mjomba kama anakereka ahame yeye.”
“Lakini kumbuka ni mama yako.”
“Ni kweli, na mimi ni mwanaye lakini nani ambaye hataki maelewano.”
Majibu yangu yalimfanya mjomba akose la kusema, moyoni niliapa sihami na kama kuhama ahame yeye.  Siku zilikatika huku nikiendelea na biashara zangu kama kawaida na uhusiano wangu na mama mdogo ukiwa mbaya tulikuwa kama chui na paka.
Sikujali kwa vile hakunizaa, tulikutana kupitia mama yangu pia hata katika maisha alikuwa hanilishi wala hanivishi. Hivyo sikufikiria kupungukiwa na kitu kama nitakosa salamu zake.
HUJUMA ZAANZA NDANI
Baada ya zoezi la awali kushindikana, mjomba alinifuata tena na kunieleza ninatakiwa kuhama kwa nguvu au kwa hiyari. Nilimweleza sitahama kwa vile sehemu kubwa ya matengenezo ya nyumba ni nguvu yangu. Nilimwambia hata yeye pamoja na kukaa Ulaya hakuwahi kutuma pesa ya kutengeneza nyumba.
Majibu yangu yalionesha kama dharau kwake na kujikuta naanzisha matatizo mengine na mjomba. Lakini ilionyesha alikuwa akinitafutia sababu nilishangaa akiniambia.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG