Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, October 17, 2014

MKALIMANI IBADA YA MANDELA AOMBA RADHI, AJIITA BINGWA

Thamsanqa Jantjie akiwa 'beneti' na Rais Barack Obama wa Marekani siku ya ibada ya Mandela.
Thamsanqa Jantjie.
MKALIMANI wa ishara za viziwi aliyeshambuliwa wakati wa ibada ya hayati Nelson Mandela amejitetea na kusema anaifahamu kazi yake vyema.
Mtu huyo, Thamsanqa Jantjie, alisema jana ana ujuzi mkubwa wa kazi hiyo na ameifanya katika matukio mengine makubwa nchini humo.
“Nimeifanya kazi hii kwa miaka mingi,” aliliambia shirika la habari la CNN na kuongeza: “Nimekuwa bingwa wa kazi hii ninayoifanya.”
Hata hivyo, mkuu wa Taasisi ya Wakalimani ya Afrika Kusini , Johan Blaauw,  amepinga maneno hayo akisema mwaka jana Jantjie alikalimani mkutano mkuu wa chama cha African National Congress na kusababisha malalamiko mengi.  Aliyasema hayo akiliambia shirika la habari la South African Press Association.
Lakini Jantjie alijitetea: “Sijawahi kuifanya kazi yangu kwa makosa,” na kuongeza: “Iwapo chama cha viziwi cha nchini, DeafSA,  wanasema nilikosea, basi naomba msamaha lakini waniambie kwa nini walikuwa kimya muda wote huu na miaka yote hii.”
Hata hivyo, Jantjie alikataa kusema nani alimwajiri katika hafla hiyo iliyochukua saa nne na kutazamwa na mamilioni ya watu duniani.  Alisema ameingia katika ukalimani kwa vile ni kilema.
“Nina matatizo ya akili, lakini ugonjwa huu unadhibitika.  Na sasa napata tiba,” alisema  Jantjie.
Katika mkutano wa waandishi wa habari jana, Hendrietta Bogopane-Zulu, Naibu Waziri wa Wanawake, Watoto na Walemavu alisema ni kweli makosa yalitendeka, lakini Jantjie si tapeli kwani hatua zote za usalama zilifuatwa.
Hata hivyo, serikali ilipogundua kampuni la mkalimani huyo, wamiliki wake walitoweka na Jantjie alipoulizwa kuhusu sifa zake alisema ziko kwenye hati za kampuni hiyo.
Chama tawala cha African National Congress kimesema hakihusiki na mtu huyo kwani hafla nzima ilikuwa imeandaliwa na serikali.
Na Jantjie alipoulizwa aliitwa na nani kwenye ibada hiyo, alisema ni mwanamke mmoja na kwamba alitumia ishara za lugha za Afrika Kusini.
Lakini wataalam wanasema jamaa huyo hakuonyesha hata ishara za sura ambazo ni muhimu kwa lugha za Afrika Kusini, na kwamba alama za mikono yake hazikumaanisha chochote

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG