Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, October 19, 2014

Rais S Leone ateua tume ya Ebola


Mwanamke anayeshukiwa ana Ebola akilia nje ya ola alia nje ya zahanati Sierra Leonene Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ameteua tume mpya ya kupambana na ugonjwa wa Ebola ambao umeuwa watu 1,200 nchini humo.
Tume hiyo mpya itasimamiwa na waziri wa ulinzi, Meja Alfred Palo Conteh., na itaripoti moja-kwa-moja kwa Rais Koroma.
Taarifa ya rais ilieleza kuwa ililazimika kufanya mabadiliko hayo kwa sababu ya kazi kubwa ilioko ya kupambana na Ebola nchini Sierra Leone.
Umoja wa Mataifa umeanza kusambaza chakula katika mji mkuu, Freetown, kwa sababu watu wengi wanaogopa kutoka nje ya majumba yao wasije wakaambukizwa ugonjwa huo.
Na Rais Obama ameonya watu wasiingiwe na taharuki kubwa kuhusu ugonjwa wa ebola na alisema kuwa Marekani haitazuwia safari za ndege kutoka nchi za Afrika Magharibi zilizoathirika na ugonjwa huo.
Rais Obama alisema hatua kama hiyo itafanya hali kuzidi kuwa mbaya.
Taarifa hiyo imetoka wakati vyombo vya habari vya Marekani vinaarifu kuwa Bwana Obama, faraghani, ameonesha hasira jinsi serikali yake ilivvyoshughulikia msukosuko huo wa Ebola.
Ijumaa, mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola, David Nabarro, alitetea juhudi zilizofanywa kimataifa kupambana na ugonjwa huo.
Bwana Nabbaro alikuwa akijibu lawama za shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF, kuwa ahadi za kimataifa za matibabu na msaada, bado hazikupunguza mfumko wa ugonjwa wa Ebola.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG