Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, October 19, 2014

Cuba yatuma madaktari zaidi kutibu Ebola

Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro, anasema nchi yake itatuma karibu madaktari na wauguzi 300 zaidi kusaidia kupambana na Ebola Afrika.

Alisema Cuba iko tayari kushirikiana na Marekani kwa masilahi ya amani duniani.
Cuba imeshatuma madaktari na wauguzi 165 huko Afrika Magharibi.
Katika tukio jengine, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa ripoti yake ya siri iliyofichuliwa nje ya shirika, ambayo ilidai kuwa shirika hilo lilifanya makosa katika kushughulikia janga hilo la Ebola, haikuwa kamilifu na ilikuwa bado haikuchambuliwa.
WHO imesema uchambuzi kamili wa hatua ilizochukua utakamilika baada ya ugonjwa wa Ebola kudhibitiwa.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG