Mathias Canal akiwa amepanga msitari na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igowole kwa ajili ya kwenda kuchukua chakula
Wanafunzi hao wakimsikiliza Mathias Canal
Wengine
husoma habari zetu, wengine hutusikiliza hivyo wanapopata nafasi ya
kuonana na wanaowasona au kuwasikiliza hakika hufurahi.
Pichani
ni wanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Igowole iliyopo
Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.Shule ambayo imeongoza kitaifa matokeo
ya kidato cha sita mwaka huu, Nimezungumza nao kuhusu mambo mbalimbali
yahusuyo elimu lakini pia tasnia ya habari.
Nilipanga
mstari wa kupata chai ya bila kitafunwa, kwani kitafunwa kila mtu
hujitegemea, nilifurahi sana maisha yale kwani yalinikumbusha miaka
kadhaa iliyopita nikiwa kidato cha tatu Nsumba Boys Jijini Mwanza kwani
tulikuwa na mlo mzuri asubuhi kwa kupata chai na skonzi 2 kila
mwanafunzi.(T.K)
Walifurahishwa na maelezo juu ya umuhimu wa habari lakini pia ugumu wa kutafuta habari.
Hakika
wanafunzi hawa wameniuliza maswali mengi hususani katika mauaji ya
Mwanahabari Daud Mwangosi aliyeuwawa Sept 2012 akiwa kazini kijiji cha
Nyololo.
Wengine
walisema wanaogopa kuwa waandishi kwa kuhofia kupigwa na polisi.Ila
niliwatia moyo kwamba kila kazi ina changamoto zake, hivyo wasikate
tamaa na kuziamini ndoto zao ile zitimie.
No comments:
Post a Comment