Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, November 1, 2014

JESHI LAGAWANYIKA KUHUSU UONGOZI BURKINA FASO


  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 

Jenerali, Honore Traore, mkuu wa majeshi ya Burkina Faso akitangaza kuchukua madaraka ya nchi.
Mgawanyiko umeripotiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso kuhusu ni nani anayefaa kuliongoza taifa hilo kufuatia kujiuzulu kwa rais Blaise Campaore baada ya miaka 27 uongozini.
Kituo kimoja cha radio kilitangaza taarifa kutoka kwa naibu mkuu wa kikosi cha kumlinda rais kanali Isaac Zida iliyosema kuwa amechukua jukumu la kuliongoza taifa hilo.

Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (katikati),akitangaza kuchukua madaraka kwa waandishi wa habari. 
Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (kati kati),akizungumza kwenyemkutano na waandishi habari kutangaza kwamba anachukua madaraka ya nchi akiwa katika makao makuu ya jeshi mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 31, 2014.
Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukaniBlaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.

Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Campaore.
Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG