Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, November 1, 2014

NEEMA CRAFTS WATOA MSAADA WA BASKELI KWA WALEMAVU.

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 
Walemavu Mkoani Iringa wakifurahia baada ya kukabidhiwa baskeli zao ikiwa ni msaada kutoka Neema Crafts
Mkurugenzi Mtendaji wa Neema Crafts Bwana Benjamin Ray akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa baskeli walioutoa kwa walemavu wa Mkoani Iringa. 
Na Simon Victor
Walemavu mbalimbali mkoani Iringa hapo jana walipewa msaada wa baskeli arobaini kutoka Neema Crafts ambao wako chini ya dayosisi ya Ruaha.
Mkurugenzi mtendaji wa Neema Crafts bwana Benjamin Ray akizungumza kwenye makabidhiano hayo alisema kuwa, Neema crafts ilianzishwa mwaka 2003 chini ya dayosisi ya Ruaha.(T.K)
Ilianza ikiwa na viziwi watatu na walikuwa wakijishungulisha na utengenezaji wa karatasi. Mwaka 2009 walijenga jengo ambalo wanalitumia kwa mgahawa na mwaka 2011 waliongeza jengo jingine ambalo wanitumia kama nyumba ya kulala wageni ambayo inasimamiwa na walemavu na kuwa nyumba ya kwanza ya kulala wageni kusimamiwa na walemavu wa kuongea(Mabubu).
Bwana Ray alisema miradi yao yote inasimamiwa na walemavu wa aina mbali mbali.Pia Ray isema msaada wa baskeli waliotoa kwa walemavu ni zawadi waliyopewa kutoka nchini Marekani katika jimbo la Minnesota.
Nae Mwenyekiti wa Walemavu(CHAWATA) mkoani Iringa Bwana Shaabani Shomari aliwashukuru Neema Crafts kwa msaada waliotoa kwao.Lakini akatatoa angalizo kwa walemavu wote waliopata baskeli hizo wazitumie kwa madhumuni yaliokusudiwa.
Pia Katibu wa CHAWATA Mkoa wa Iringa Ndugu, Haruna Mbata amewapongeza Neema Crafts kwa kuwa bega kwa bega na wao na msaada waliotoa ni chachu kwa maendeleo ya walemavu Mkoani Iringa

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG