Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, November 1, 2014

Wakulima wa mpunga Igurusi waomba wataalamu wa kilimo


Walisema wakulima wengi wanalima kilimo cha kizamani ambacho hakina tija kutokana na ukosefu wa wataalamu vijijini 
Kwa ufupi
“Tunaiomba Serikali itusaidie sisi wakulima wadogo wadogo wa zao la mpunga vijijini kutufikishia utaalamu wa kilimo ili tuweze kupatiwa elimu ya shamba darasa na tujikite zaidi katika kilimo bora,” alisema.

BAADHI ya wakulima wa zao la mpunga wilayani Mbarali, mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwafikishia wataalamu wa kilimo ili waweze kuwapatia elimu ya kilimo bora cha kisasa kwa nia ya kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao mengi.

Wakizungumza jijini hapa jana wakulima kutoka Kata ya Igurusi walisema kuwa uelewa mdogo na kutozingatia kanuni bora za kilimo ni chanzo cha kutopata mazao mengi ya chakula na biashara.

Walisema wakulima wengi wanalima kilimo cha kizamani ambacho hakina tija kutokana na ukosefu wa wataalamu vijijini.Akizungumza kwa niaba ya wakulima, Amos Matanana alisema uelewa mdogo wa kuzingatia kanuni bora za kilimo ni chachu kwao na kwamba ni wakati wa Serikali sasa kuwasaidia wakulima vijijini kufikiwa na wataalamu wa kilimo, ili waweze kupatiwa elimu ya kupanda mazao kwa kuzingatia kanuni za kilimo cha kisasa.

“Tunaiomba Serikali itusaidie sisi wakulima wadogo wadogo wa zao la mpunga vijijini kutufikishia utaalamu wa kilimo ili tuweze kupatiwa elimu ya shamba darasa na tujikite zaidi katika kilimo bora,” alisema.

Alisema wakulima wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi hususan kipindi cha msimu wa kilimo ukosefu wa skimu za umwagiliaji na kwamba hali hiyo imekuwa ikichangia wakulima kutopata mazao mengi katika msimu wa mavuno.

Aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwafikishia mikopo ya matrekta madogo (powertiller) ili waweze kuzalisha zao hilo kwa wingi na kupata soko la uhakika litakaloweza kuwakwamua kiuchumi.Wakati huohuo wakulima waliopata pembejeo za ruzuku wameitaka Serikali kuzingatia muda wa kupanda na kutumia mbolea ya kupandia ili kuepuka kupeleka mbolea katika muda usiofaa.
Rai hiyo ilitolewa kufuatia kupelekewa mbegu wakati muda wa kupanda umepita.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG