Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, November 12, 2014

LIBYA WATATU WACHINJWA KWA MAONI YAO


  • Share on facebook
    Share on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Mjini Derna, kundi la Is limeshika hatamu
Wanaharakati watatu wa kisiasa nchini Libya wamechinjwa baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya kiislam.Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna karibu na Benghazi.
Tukio hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu.Mji huo wa Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka 2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la is.
Mnamo mwezi August mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani katika viwanja vya mpira mjini Derna.
Siku za hivi karibuni kuna picha iloachiliwa mitandaoni ikionesha kikundi cha kijamii kinachojiita mahakama ya kiislam.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG