Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, November 12, 2014

NIGERIA:WANAFUNZI 47 WAUAWA SHULENI


  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakishambulia eneo hilo la Potiskum
Kumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Duru zinasema kuwa wanafunzi 47 wameuawa katika shambulizi hilo linalosemeklana kufanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa amevalia sare za shule.
Shambulizi lilitokea wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji wa Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.
Shule hiyo ni ya mafunzo ya sayansi. Mwalimu mmoja alinukuliwa akisema kuwa alisikia mlio mkubwa wa kutisha wakati bomu hilo lilipolipuka.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG