Katika Mkoa wa Dar es Salaam upo ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali kwa wanyama wakubwa na wadogo, kwa ajili ya chakula , biashara, wanyamakazi na wanyama rafiki (pets). Shughuli za ufugaji zinafanyika kwa idadi maalum kutegemeana na aina ya mifugo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Aidha ufugaji huu unasaidia kwa kiwango kizuri kutoa ajira kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ufugaji huu unatakiwa uwe endelevu na wenye kuzingatia kanuni za ufugaji bora.
|
No comments:
Post a Comment