Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, November 16, 2014

TANZANIA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA SEKTA YA NYUKI DODOMA

index
Mahmoud Ahmad Arusha
Tanzania  inatarajia kujenga kituo Kikubwa   cha sekta ya nyuki ambacho kitatoa mafunzo  juu  ya namna bora ya kufuga nyuki kisasa
Mtendaji Mkuu wa baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi Dakta  Anaclet Kashuliza  ameeleza hayo  wakati wa kongamano la kwanza  la ufugaji nyuki barani Afrika.
Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa MKoani Dodoma kwa msaada wa Kampuni moja kutoka Marekeni mbali na kituo hicho kuhusika na utoaji  mafunzo pia kitahusika na  uchakataji  wa asali
Dakta Kashuliza amesema kuwa kituo hicho  kitahusika na utunzani wa  kumbukumbu  ya vitu vya  asali  vya ufugaji nyuki hapa Tanzania na kinatarajia kuanza katika kipindi cha miezi minne ijaayo
Dakta Kashuliza  aidha amesema mbali na kujengwa kwa kituo hicho kikubwa barani afrika pia  Tanzania inatarajia kujenga viwanda vidogo vidogo, vya kati na viwanda vikubwa kwa ajili ya kusindika asali na nta
Viwanda hivyo  vitatumika kwa ajili ya watalii kutoka nje  watakaopata fursa ya kutembelea viwanda hivyo pamoja na kituo kikubwa  cha  Dodoma kujionea  juu ya hali ya raslimali asali ilivyo.
Wakati huo huo Serikali Mkoa wa  Singida imesema kuwa ipo tayari  kuyaondoa  makundi yote  ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent  Parseko  Kone
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao  ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama  jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa   asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima  jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao  maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki 
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia  Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga  zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia  mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
Mkoa huo hivi sasa una  watu wapatao 1,300 wa jamii ya  wahadzabe ambapo  300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki  ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo  vya  baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa  kutumia nguvu  za kiuchumi walizonazo
Hivyo ameitaka   serikali kuhakikisha  jamii   ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika  baadhi ya maeneo
Amekiri kuwa  kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa  hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi

Serikali Mkoa wa  Singida imesema kuwa ipo tayari  kuyaondoa  makundi yote  ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent  Parseko  Kone
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao  ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama  jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa   asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima  jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao  maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki 
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia  Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga  zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia  mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
Mkoa huo hivi sasa una  watu wapatao 1,300 wa jamii ya  wahadzabe ambapo  300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki  ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo  vya  baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa  kutumia nguvu  za kiuchumi walizonazo
Hivyo ameitaka   serikali kuhakikisha  jamii   ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika  baadhi ya maeneo
Amekiri kuwa  kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa  hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi
Hatua hii itachangia kuvutia zaidi masoko ya nje kutokana na watalii hao kutembelea viwanda hivyo
Aidha Dakta Kashuliza amesisitiza kuwa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi limejipanga  kuimarisha elimu kwa wazalishaji na  wafugaji wa nyuki ili waweze kuzingatia  uzalishaji wa  asali katika viwango vyenye ubora kimataifa
Elimu hiyo itatolewa na baraza hilo kwa ushirikino  na TBS ili kuwezesha asali ya Tanzania kupata masoko ya uhakika nje ya nchi.amesisitiza Katibu Mtendaji huyo  wa baraza hilo
Mbali na hatua hiyo Dakta Kashuliza amesema Baraza  limeanzisha Programu ya majaribio katika miko 10 ya Tanzania bara kuhisiana na ufugaji nyuki ili  wafugaji hao waweze kufuga kiisasa zaidi na kibiashara katika viwango vyenye ubora kimataifa
Dakta Kashuliza ameitaja mikoa inayotekeleza Programu hiyo ya majaribio kuwa ni Mkoa wa Pwani,Dodoma,Morogoro,Tanga,Manyara, Iringa, Singida, Tabora Katavi na Kigoma
Amesema baraza  hivi sasa linasimamia  kwa nguvu zote suala la wafugaji kutumia teknolojia  bora zaidi katika ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga bora
Mbali na hatua hii Baraza pia limeingia mikataba na  wadau mbalimbali wa nje ya nchi ili kuwaunganisha wazalishaji wa asali nan je kuweza kupata masoko ya uhakika ya mazao ya nyuki kutoka Tanzania.Amesisitiza Dakta Kashuliza

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG