Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, November 16, 2014

TUMETOKA MBALI: MIMI NA KAKA YANGU MUHIDIN ISSA MICHUZI...!


  • Share on facebook
    Share on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Ndugu zangu,
Mara ya kwanza kulifahamu jina Muhidin Issa Michuzi ilikuwa ni pale Tambaza Sekondari, ni mwaka 1986, nilikuwa Kidato cha Tatu. Tayari wakati huo nilikuwa na kijarida changu ' Tambaza News' nilichokuwa nikikiandika kwa mkono kwenye A4 na kubandika kwenye ubao wa matangazo. Nilikuwa na wasomaji wengu akiwamo Makamu Mkuu wa Shule, Mr. Mwaipopo.
VICTOR SIMON
Jumamosi moja niliangalia kwenye gazeti la Mfanyakazi nikakutana na picha iliyopigwa Mtaa wa Msimbazi ikionyesha ghorofa lililoporomoka kutokana na kukosa viwango. Na ni nani basi aliyekuwa wa kwanza kufika hapo kurekodi tukio hilo?
Ni Muhidin Issa Michuzi!
Nami nilikuwa mpenzi sana wa kupiga picha tangu utotoni. Nikajiuliza ni nani huyu Muhidin Michuzi? Miaka mitano baadae nikakutana nae pale Daily News. Niliyekuwa nikiwafuatilia kabla ya hapo ni Joseph Milinga aliyekuwa akipiga sana picha za michezo. Pale Karume Stadium, ningali mtoto, nilipenda sana kumfuatilia Milinga akiwa anawinda picha uwanjani. Ndiye aliyenifanya nianze kusoma Daily News mapema kwa vile picha za Milinga zilichapwa kwenye Daily News. Mwingine alikuwa Vicent Urio, sidhani kama katika nchi hii ametokea mpiga picha mahiri kama Vicent Urio ukimwacha kaka yangu Muhidin Michuzi.
Na nini ni special kwa Michuzi?
Michuzi ana 'Jicho la picha'. Kupiga picha ni sanaa. Mpiga picha mzuri ni yule mwenye ' Jicho la Picha'.
Vinginevyo, unaweza ukabeba kamera yako na kutembea kutoka Kinondoni hadi Kariakoo usione hata picha moja. Na ukijilazimisha kupiga basi itakuwa unapiga 'picha bubu'- Picha zisizoeleza chochote.
Good morning!
Maggid,
Iringa

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG