Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao kwa mwaka 2014. Takribani wahitimu 3459 wametunukiwa Astashahada, Shahada na Stashahada za fani mbalimbali.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi rasmi wa mahafali hayo jijini Dar es salaam. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Mathew Luhanga (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema.Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu 3459 wa fani mbalimbali wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao mwaka 2014.Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)Prof. Mathew Luhanga akizungumza na wahitimu hao.Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akisoma tamko la kuwatunuku wahitimu 3495 wa fani mbalimbali wa chuo cha CBE wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment