Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, November 5, 2014

UPISHI NI CHANZO CHA MARADHI


  • Written by  Mjengwa Blog 
  • Email 
  • Tuma Maoni 
  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Je, unamjua mnyama aitwaye Nyani? Kama humjui tembelea mbuga za wanyama au mapori makubwa. Ila kama ni kwa ajili ya gumzo letu leo basi tafuta hata picha yake umwangalie vizuri.
Wiki hii Mtaalamu wa tafiti na tiba zinazohusiana na lishe Dr. John Haule ambaye pia ni mmiliki wa kituo Kiitwacho HerbHunter kilichopo jijini Dar Es Salaam aliweka 'mambo hadharani' kupitia mtandao bora wa habari nchini, Global Publishers ambao ni ndugu wa gazeti hili kwa kuwaasa watanzania na dunia kwa ujumla kupunguza matumizi ya moto katika maandalizi ya vyakula. Akiongea ofisini kwake alithibitisha kuwa ugunduzi wa moto duniani ndio uliopelekea afya za watu wote duniani kuwa mashakani kwani licha ya kemikali kama chumvi, sukari na mafuta kuwemo katika list hiyo ya vyanzo vya maradhi Dr. John alisisitiza kuwa moto ndio unaoongoza kwa kusababisha maradhi yasiyotibika takriban yote duniani.(Martha Magessa)
Dr. John alianza kwa kusema " Waone Nyani, wao hawaugui kama binadamu na neno hospitali kwao ni msamiati mkubwa sana. Wao huugua maradhi ya mlipuko na majeraha tu. Shida kubwa kwao ni kuliwa na wanyama wakali tu yaani 'predetors'. Hawaugui kwa sababu wao hawapiki chochote kiingiacho midomoni mwao. Kifupi wao hula vyakula asili yaani 'natural state foods' hivyo hukutana na madawa halisi yoote ambayo ndio ilikuwa hospitali na zahanati ya bustani ya Eden ambapo Adam na Eva waliishi miaka mingi bila kuugua. Cha ajabu, binadamu mwenye werevu kuliko viumbe wote duniani hupika vyakula ambavyo huunguza madawa hayo yote na bahati mbaya zaidi vyakula vingi hugeuka sumu na kumdhuru binadamu bila yeye kujijua, mfano rahisi nit u ni kwamba 'calories' huongezeka mara nyingi sana katika vyakula na kuwa chanzo cha ugonjwa wa kisukari na unene wa kupindukia pia na hivyo kuufanya moto kuonekana kama muuaji mkubwa sana asiyeonekana duniani yaani 'invisible predetor' ambaye anadhibitika kirahisi mno kwa kula vyakula visivyopikwa."
Dr. John alimalizia kwa kusema "Ni vigumu mno kula nafaka kama mahindi nk kama alavyo nyani hivyo ni bora tukapunguza ulaji wa vyakula vinapikwa na kuongeza mezani vile visivyopikwa kama vile kachumbari, matunda, juisi za matunda halisi na saladi pia kwa asilimia 75% hadi 80% ya kila mlo uingiao midomoni mwetu na hakika baada ya mwezi mmoja wengi wetu tutapona maradhi mengi sana. Wapo walio taabani kwa maradhi kama vile waliopo mawodini ambao pamoja na vyakula hivyo bado wanahitaji "multivitamins" ambazo huharakisha uponyaji kwa kuwa zimetengenezwa kitaalamu zaidi katika maabara zinazozingatia ubora" Alimalizia Dr. John ambaye ni mtaalamu wa tiba za lishe yaani Food Therapy aliyeidhishwa na Kampuni ya kutengeneza virutubisho Afrika Kusini iitwayo Nativa kupitia Afya Distributors ya Jijini Dar Es Salaam.
Hizi ni taarifa njema sana kwa yeyote Duniani. Jitahidi kufikisha ujumbe huu kwa watu wengi zaidi uwezavyo ili tuokoe afya za Watanzania na Dunia kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa gharama za matangazo yatakayopelekea wagonjwa kusikia hii habari yanagharimu pesa nyingi na kituo cha HerbHunter pekee hakiwezi kumudu gharama za matangazo hayo hasa ikizingatiwa kuwa matangazo ya magazetini na redio ndio yenye kuwafikia watu wengi zaidi kwani tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia kama 20% tu ya watu duniani hupata taarifa kupitia mitandaoni. Kwa wenye maradhi kama Presha, Kisukari na vidonda vya tumbo ningewaomba wafike kuniona haraka kwa sababu tayari dawa imepatikana na wengi tu tayari wameshanufaika. Unaweza kulisoma tangazo la tiba hii katika ukurasa wa LOKOPROMO tangazo la (HERBHUNTER) katika gazeti la NIPASHE la wiki hii yote kwa uhakika zaidi. Ukiwa na swali, hoja, maoni au ushauri basi usisite kutupigia kwa namba 0768 215 956 na karibu sana utembelee mtandao wetu wa Global Publishers.
John Haule
0768 215 956

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG