HUMPHREY POLEPOLE KIONGOZI WA VIJANA |
Kama wageni wanauona utajiri huo je wewe unaye lia njaa wakati upo bize na vijibarua vya mjini ambavyo haviwezi kukukimu wewe je utawezaje hata kuwa na familia ,sasa ni wakati wakushughulikia ipasavyo fursa zilizopo katika maeneo yetu hasa vijijini hapa napo wadau wa maendeleo hasa serkali,mashirika binafsi,tuwekeze vijijini ,leo si ajabu kusikia nina shirika la kilimo na nipata misaada kusaidia wakulima wadogo elimu wakati hilo shirika lipo mjini tunashangaa hao walengwa wako wanalima nini lami au kilimo cha ndani ya nyumba.
Ukweli uliopo hakuna mjanja wa karne hii kama kijana anayeweza kutumia vema muda na mazingira yake vizuri kwani hatajuta kwaajiri ya muda nakujiua eti maisha magumu,wakati huu ni hatari sana kuwa na rafiki anaye kushauri kushinda vijiweni eti ni sehemu bora kama ni mahali safi kwa mawazo basi maamuzi ya mataifa yangefanyika huko ,watanzania vijana tubadilike na tuingie kwenye mapambano ya wakati uliopo.
Anayehitaji kushinda lazima apambane ni si kupambana tu bali kuangalia mbele hapa namaanisha kuwa na malengo ambayo yatakupa nguvu ili usibabaishwe na kelele za watu na wengine kufikia kukutenga kwa kuwa na msimamo wako imara kwani utakapo fanikiwa na na wao utawasaidia lakini ukiwasikiliza na mwishowe ukashindwa kuwasidia wata kulani milele.
MHE ;JOHN MNYIKA[ MBUNGE ]KIJANA |
Basi ni muda wa vijana kujiona kuwa ni sehemu ya dunia na jamii intuhitaji tena kwa kiwango kikubwa sana kuliko vile tunavyojiona ili tuweze kukumboa nchi zetu hasa za dunia ya tatu sasa sisi tukijiremba wakati ndugu zetu wanakufa kwa njaa,kukosa matibabu,vita, na utapiamlo ni aibu kubwa kwani wazee wetu walipigana wakatulea leo wao watakuffa kwa aibu ni dhambi kubwa kwa muumba wetu.
No comments:
Post a Comment