Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, December 13, 2014

BASATA KUWAPIGA MSASA WAIMBAJI DESEMBA 17

imagesNa Mwand Wetu
WAIMBAJI watakaoimba kwenye Tamasha la Krismasi katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea  wanatarajia kupigwa msasa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kupitia semina itakayofanyika Desemba 17 katika ofisi za Msama Promotions, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abihud Mang’era semina hiyo itahusisha baadhi ya watendaji  wa Basata ambao watafikisha ujumbe wa serikali katika tasnia ya muziki.
Mang’era alisema ni muhimu kwa waimbaji kuhudhuria semina hiyo ambayo ina lengo la kuwapa mwangaza waimbaji ambao watashiriki kutoa huduma ya neno la Mungu.
“Ni muhimu kwa waimbaji kuhudhuria katika semina hiyo ambayo itaongozwa na watendaji wa Basata ambao watashirikiana na watendaji wa Msama Promotions,” alisema Mang’era.
Mang’era alisema semina hiyo itawasaidia waimbaji kukumbuka masuala ya msingi pindi wawapo jukwaani  ambako alisisitiza waimbaji kuhudhuria semina hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG