Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, December 1, 2014

JB NAWEZA KUWA KAMA ZAMANI

MKONGWE wa filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’ amefunguka kwamba anaweza kuuweka kando ubonge na kurejea kwenye muonekano wake wa zamani kama atatakiwa kuwa hivyo.Mkongwe wa filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’ akila tizi.
JB aliyasema hayo alipoulizwa kuhusiana na picha yake ya zamani inayomuonesha akiwa mwembamba sana tofauti na ubonge alionao sasa ambapo alijitetea kwamba yeye ni msanii na filamu ndizo zinazomweleza awe katika muonekano gani.
“Mimi siwezi kujipangia niwe katika muonekano gani isipokuwa filamu ndiyo inanipangia ikitaka niwe mwembamba kama zamani nitapunguza kilo kwa kufanya mazoezi na ‘diet’ ili niendane nayo,” alisema JB.
Picha hiyo ya zamani ilionekana kuwashangaza wadau mbalimbali mtandaoni na kutoa maoni yao kwamba kweli wameamini hakuna mtu mwembamba duniani.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG