Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 17, 2014

Mradi wa MUVI kuunda ajira zaidi ya mia moja

Mradi wa MUVI kuunda ajira zaidi ya mia moja

Mradi wa MUVI unatarajiwa kuongeza ajira zaidi ya mia moja (100) kwa vijana wa wilaya za Handeni, Korogwe na Muheza. Hii ni kufuatia mafunzo ya kusafisha mashamba yanayotolewa na mradi huu katika vikundi vya Wilaya hizi tatu.
Mafunzo haya ambayo yanalenga kuwaandaa vijana wa umri wa kati ya miaka 30-40 kuweza kuhudumia mashamba ya mIchungwa kwa kuyafanyia usafi wa mara kwa mara ili kudhibiti nzi mharibifu wa matunda yanahusisha kukata matawi yasiyofaa katika miti ya michungwa (prunning), kufyeka majani yote shambani na kufukia machungwa yaliyoanguka ili kupunguza mazalia ya nzi hawa.
Pichani: Ndugu Paulo Kadaga akifanya majaribio ya kufyeka kwa mashine maalumu ya kufyekea.
Mafunzo hayo yamekwisha anza Wilayani Muheza ambapo vijana watano katika kila kikundi kinachofanya kazi na mradi wa MUVI watapatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mashine maalumu ya kufyeka nyasi na matawi madogo. Vijana hawa wanatarajiwa kuifanya shughuli hii kuwa ajira yao ya kudumu kwani kila kikundi kitapatiwa mashine moja na vijana hawa wataitumia katika mashamba ya wakulima na kulipwa kutokana na kazi hii, pesa itakayopatikana kutokana na kazi hii nusu itaingia kwenye mfuko wa kikundi na nusu atapewa kijana aliyefanya kazi husika.
 Zoezi hili linafuatia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na kikosi kazi cha kupambana na nzi waharibifu wa machungwa kinachojumuisha wadau mbalimbali wa zao la machungwa katika mkoa wa Tanga sambamba na mradi wa MUVI.
Mradi wa MUVI umeunda kikosi kazi hiki ili kugawana majukumu baina ya wadau wengine wa machungwa wakiwemo wauzaji madawa ya kilimo, watendaji wa halmashauri ya wilaya, wana habari na mradi wenyewe ili kutokomeza kabisa tatizo la nzi wa matunda. 
Nzi huyu ambaye anatagia katika matunda hususan machungwa na maembe aliliripotiwa kuwepo hapa nchini mnamo mwaka 2003 akitokea nchi jirani ya Kenya.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG