Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 17, 2014

Mvua yaathiri alizeti

Mvua yaathiri alizeti

Wakulima wa zao la Alizeti katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wameathirika kutopata alizeti msimu huu kutokana na kuchelewa kwa mvua.
Wakizungumza na afisa habari wa mradi wa Muunganisho ujasiriamali vijijini (MUVI) mkoa wa Mwanza Ndugu Eva Mushi kwa nyakati tofauti, afisa kilimo wa kata ya Ilangala Wilayani Ukerewe, Bwana Abito Ngereza amesema, kitaalamu, alizeti katika wilaya ya Ukerewe huoteshwa kati ya mwezi wa kwanza tarehe kumi na tatu hadi tarehe kumi na tano mwezi wa pili.
Tarehe hizo kulikuwa na kiangazi ambapo wakulima hawakuotesha. Mvua zilianza kunyesha kidogo mwezi  wa nne ambapo wakulima waliotesha na kwa kuwa msimu wa kupanda ulikuwa umepita mbegu hazikuota ipasavyo na walirudia mara mbili bila mafanikio, hivyo wakulima katika kata ya Ilangala msimu huu hawatopata alizeti.
Katika kata ya Nduruma, ukosekanaji wa mvua kwa muda wa kuotesha alizeti napo wameathirika. Bwana Samson Tengule ambaye ni mwanakikundi wa mradi wa Muvi katika kikundi cha Bure Garden amesema wamejitahidi kuotesha alizeti baada ya mvua kidogo kunyesha lakini alizeti haikuota ipasavyo, imewabidi kurudia mara mbili ndipo mbegu zikaota japo moja moja na sehemu nyingine hazikuota kabisa. Kutokana na hali hii katika kata ya Nduruma upatikanaji wa alizeti msimu huu utapungua kwa kiasi kikubwa tofauti na msimu uliopita.
Uoteshaji wa alizeti katika kata za Malegea na Namagondo na kata nyingine haukuwa mzuri kabisa kutokana na hali ya ukame na mvua kutonyesha kwa muda tarajiwa wa kuotesha alizeti.
Afisa kilimo wa kituo cha utafiti Ukiriguru mkoani Mwanza, Bwana Bujiku Ngereza, amesema pamoja na kuwa msimu wa kuotesha alizeti katika wilaya ya ukerewe ulibadilika kutokana na uhaba wa mvua, hata hivyo wamechukua sampuli ya mbegu zilizotolewa katika wilaya hiyo na wanazifanyia utafiti ili kujua kama tatizo lilikuwa la mbegu maana wameingia na wasiwasi kuona hata zile mbegu wakulima walizootesha wakati mvua zilipoanza kunyesha mwezi wa nne nazo hazikuota kabisa.
Katika wilaya nyingine mkoani Mwanza hususan wilaya zilicho chini ya mradi wa MUVI, wilaya za Kwimba na Sengerema alizeti inaendelea vizuri na wanatarajia kuvuna kuanzia mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG