Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 17, 2014

Muhogo

Muhogo

Muhogo ni mmea unaotumika kwa ajili ya chakula hivyo kuwa zao muhimu katika Afrika hususan Tanzania.
Sehemu inayoliwa  hasa ni mizizi yake minene iliyo na wanga mwingi na majani yake yenye hutumiwa kama mboga iliyojaa protini na vitamini.
Kuondoa Sumu ndani ya aina za muhogo
Kuna aina kadhaa za muhogo zinazolimwa hapa Tanzania na  hutofautiana kwa ladha tamu au chungu na hasa kwa kiwango cha sianidi (cyanid) ndani yake. Sianidi ni sumu iliyo ndani ya mmea kwa umbo la kemikali ya linamarin. Linamarin hubadilika kuwa sianidi.
Viwango vya sianidi vinatofautiana kati ya jamii mbalimbali za muhogo. Aina zenye kiwango kidogo sana hazina matatizo lakini kwa jumla zao linatakiwa kuandaliwa kabla ya kuliwa.
Dawa ya sianidi hupotea kwa kuacha mizizi katika maji kwa siku mbili tatu ili kupata unga. Njia nyingine ni upishi kwa joto kali kwa mfano kukaanga katika mafuta. Njia nyingine inayotumiwa hasa Afrika ya Magharibi ni kusaga mizizi na kukoroga unga katika maji; baada ya masaa kadhaa maji hubadilishwa na uji unapikwa kuwa aina ya ugali.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG