Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, December 7, 2014

NCHIMBI ACHOMOZA TAMASHA LA KRISMASI SONGEA

habari2
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Songea, Dk Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi Wilayani Singea mkoani Ruvuma linalotarajia kufanyika Desemba 28 kwenye uwanja wa Majimaji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama Nchimbi amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lengo lake ni kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
“Nchimbi amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Krismasi mkoani Ruvuma, hivyo wadau wa muziki wa Injili wajiapange vilivyo kwa lengo la kupata uinjilishaji, utakaofanywa na maaskofu na waimbaji,” alisema Msama.
Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Desemba 26 litafanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Msama alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujitokeza kwa wingi kwani tamasha hilo lina lengo la kufanikisha matakwa ya wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG