Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, December 13, 2014

Nitaendelea na timu ya McLaren:Jenson

Jenson Button
Dereva Jenson Button, wa timu ya McLaren, anamatumaini ya kuendelea kuitumikia timu hiyo zaidi.
Jenson Button, amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka na timu hiyo mpaka 2016.Button amechaguliwa kuwa timu moja na nyota Fernando Alonso. "kuwa na timu ya Mclaren, kwa Zaidi ya mwaka mmoja ni muhimu ,ila niko hapa kwa ajili kupamba na michuano ya dunia” Button mwenye miaka 34 awali alionyesha kuchanganyikiwa na ucheleweshwaji wa kutatua mustakabali wake katika timu Mclaren. Mwenyekiti Ron Dennis, ameeleza ilichukua muda kuamua kati ya Button, na mchezaji mwenzake Kevin Magnussen, nani atashirikiana na Alonso, ila ikafikiwa muafaka kwa Button kuchaguliwa. Timu ya McLaren imewatangaza Jenson Button ,Fernando Alonso na Kevin Magnussen kuwa madereva wa timu hiyo kwa msimu ujao wa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG