Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, December 15, 2014

SUMAYE KUBARIKI TAMASHA LA KRISMAS MBEYA

indexNa Mwandishi Wetu
 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa Tamasha la Krismas Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda vizuri.
 
“Tulikubaliana katika kamati tumuombe Waziri Mkuu mstaafu Sumaye aje atupe baraka kwenye tamasha la Krismasi, nafurahi kusema ni mtu wa watu, amekubali kujumuika na wadau wengine siku hiyo. Hili ni jambo la furaha kubwa kwetu.
 
“Wasanii mbalimbali tunaendelea kuzungumza nao kuhakikisha wanashiriki katika tamasha hilo,”  alisema Msama katika taarifa yake.
 
Sumaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005, akiwa ndiye Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu katika wadhifa huo kwa historia ya Tanzania.
 
Alisema wamepanga kufanya maboresho makubwa katika tamasha hilo na moja ya maboresho hayo ni kuweka kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
 
“Waimbaji wote maafuru wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
 
“Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho,” anasema. Baada ya onesho la Desemba 25 mkoani Mbeya, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Desemba 28 Uwanja wa Majimaji Songea.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG