Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, December 7, 2014

Watu kadha wauwawa karibu na Beni DRC

Wanajeshi wa DRC wakielekea kwenda kupigana na ADF
Inaarifiwa kuwa watu kama 30 waliuwawa katika mashambulio kwenye vijiji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Inaarifiwa kuwa mashambulio hayo yalifanywa Jumamosi usiku kwenye vijiji karibu na mji wa Beni ambako watu zaidi ya 250 wameuwawa tangu mwezi Oktoba.
Wakuu na mashirika ya raia yanawalaumu wapiganaji kutoka Uganda wa kundi la ADF, lakini baadhi ya wadadisi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuhusisha kundi hilo

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG