Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 27, 2015

Droo ya Europa Ligi kupangwa leo

Michezo ya mtoano kufanyika March 12
Matokeo ya upangwaji wa droo ya timu 16 ya ligi ya Europa zitafanyika leo nchini Uswisi kuanzia saa tisa kwa saa za Afrika Mashariki.
Droo hiyo itasimamiwa na Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, na Mkurugenzi wa Mashindano wa UEFA, Giorgio Marchetti, pamoja na Jerzy Dudek, Kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Poland, ambae ndiye Balozi wa fainali ya Mwaka huu ya Europa Ligi itakayochezwa huko Poland, Mei 27.
Droo hii itahusisha timu 16 zilizofuzu toka kwenye timu 32 ambapo jana usiku zilikamilisha michezo yao ya marudiano.
Michezo ya mtoano itapigwa kuanzia Machi 12 na Marudiano Machi 19 na Washindi kutinga hatua ya Robo fainali.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG